Friday, May 11, 2018

Mzee wa Miaka 104 Aliyeomba Kujiua, Hatimaye Afanikiwa Kujiua




Mwanasayansi David Goodall amehitimisha safari yake ya hapa duniani baada ya kujichoma sindano mwenyewe ya sumu iliyochukua dakika moja kuchukua uhai wake.

Mwanasayansi huyo mwenye miaka 104 aliyehitimisha maisha yake ya kuishi hapa duniani alizaliwa jijini London Aprili mwaka 1914 ikiwa ni mwezi mmoja kabla ya kuanza vita ya kwanza ya dunia.

Mwanasayansi huyo mkongwe alisafiri kutoka Australia mpaka Basel, Uswis kwa ajili ya kujitoa uhai kwa hiari, ingawa alisema anachukizwa na kitendo hicho.

Goodall alishika bomba la sindano yenye sumu na kusukuma kwenye mwili wake, na ilitumia dakika moja sumu ikaenea mwili na kupoteza uhai wake.

Sindano ambayo aliitumia kujichoma ilikuwa na sumu aina ya Sodium pentobarbital ambayo iliingia kwenye mishipa ya mwanasayansi huyo.

Wasamaria wema walimchangia Dola 20,000 za Marekani ambazo ni sawa na Sh45milioni ili kumsaidia kutimiza azma yake hiyo.

Kabla ya kifo chake alisema kwamba kinachomfanya aharakishe kufa ni kutokana na kupungua kwa uhuru unaosababishwa na umri.

Hata hivyo mwili wake utachomwa moto nchini Uswisi na kisha majivu yatapelekwa nchini Australia.

Labels:

Friday, May 4, 2018

Hatimaye Mwanasayansi Aanza Safari ya Kujitoa Uhai



Mwanasayansi mwenye umri wa miaka 104 David Goodall ameaga nyumbani Australia kuanza safari ya kimataifa kwenda kujitoa uhai.

Sio kwamba mwanaekoljia huyo anaugua mahututi, La, anatamanai kuharakisha kifo chake. Sababu kuu ya uamuzi wake anasema ni kupungua kwa uhuru wake.

"Najuta kufika umri huu," Dkt Goodall alisema mwezi uliopita katika sherehe ya kuzaliwa kwake, katika mahojiano na shirika la utangazaji la Australia.

"Sina raha. Nataka kufa. Sio jambo la kuhuzunisha, kinachohuzunisha ni kwamba mtu anazuiwa kufa."

Ni jimbo moja pekee Australia lililohalalisha kujitoa uhai mwaka jana kufuatia mjadala mkali uliozusha mgawanyiko, lakini ili mtu kuruhusiwa, ni sharti awe anaugua mahututi.

Dkt Goodall anasema atasafiri kwenda katika kliniki moja nchini Uswisi kujitoa uhai kwa hiari. hatahivyo anasema anachukizwana kwamba anaondoka nyumbani ili aweze kufanya hivyo.
  • Uswizi, ni nchi pekee iliyo na vituo vinavyotoa huduma hiyo kwa raia wa mataifa mengine.
  • Uholanzi, Ubelgiji na Luxembourg zinaruhusu, hata kwa watoto lakini katika hali maalum.
  • Colombia inaruhusu kujitoa uhai kwa hiari wakati mgonjwa akiwa hatibiki.
  • Majimbo sita ya Marekani - Oregon, Washington, Vermont, Montana, California na Colorado - zinaruhusu kwa wagonjwa mahututi wasio tibika.
  • Canada ililifuata jimbo la Quebec kuruhusu hilo mnamo 2016.

Katika nchi nyingi tu Afrika, njia zote za kujitoa uhai zinatizamwa kama mauaji.

Wataalamu barani Afrika wamepinga wito wa watu kutaka kujitoa uhai kwa hiari.

Mjadala mkubwa umezuka kuhusu kinachotajwa kuwa 'kuuawa kwa huruma' hususan kwa wagonjwa walio mahututi na wasioweza kutibika.

Lakini mkutano wa muungano wa wataalamu wa afya duniani katika mkutano mapema mwaka huu mjini Abuja Nigeria waliamua kwamba hatua hiyo inakwenda kinyume na kiapo cha matabibu na inakwenda kinyume na imani na maadili ya jamii za Kiafrika.

Badala yake viongozi katika muungano hao wameyaka kuboreshwa kwa huduma za kuwashughulukia wagonjwa mahututi wasioweza kutibika.

Masuala yaliozingaiwa katika kuptisha uamuzi huo ni sheria, dini, jamii na tamaduni, saikolojia na upana wa maadili kuhusu suala hilo.

Wataalamu wa mataifa kutoka Afrika kusini, Kenya, Botswana, Zambia na Cote D'ivore walipinga hoja hiyo ya kujitoa uhai kwa hiari wakisisitiza inakwenda kinyume na maadili ya utoaji matibabu.

Labels:

Friday, April 13, 2018

Mtoto azaliwa miaka 4 baada ya wazazi wake kufariki




Mtoto amezaliwa China kupitia mwanamke aliyebeba uja uzito, miaka minne baada ya wazazi wa mtoto kufariki ktaika ajali ya gari, vyombo vya habari China vinaripoti.

Wazazi hao waliofariki mnamo 2013, walitoa mayai kadhaa yaliogandishwa kwa matumaini kwamba watazaa kupitia mfumo wa IVF.

Baada ya ajali wazazi wao waliwasislisha kesi kuruhusiwa kuyatumia mayai hayo.

Mtoto huyo mchanga wa kiume alizaliwa Desemba kupitia mwanamke aliyebeba mimba huko Laos na kisa hicho kiliripotiwa kwa mara ya kwanza wiki hii na gazeti la The Beijing News.

Gazeti hilo limeeleza jinsi hakujawahi kushuhudiwa kesi ya aina hiyo na ndio sababu iliyowalazimu wazee wa wazazi wa mtoto huyo kuwasilisha kesi kabla ya kuanza mpango wa kutafuta mbebaji mimba hiyo.
Kisa cha kwanza cha aina yake

Wakati wa ajali hiyo, mayai yalikuwa yamehifadhiwa vizuri katika hospitali huko Nanjing na yalikuwa yamegandishwa katika nyuzi joto ya chini ya 196 katika tanki lililojaa gesi lya maji ya NItrojini.

Kesi hiyo mahakamani iliwaruhusu bibi na babu wa mtto huyo kumiliki mayai hayo yaliogandishwa.

Hakukuwepo kesi ya aina hiyo awali kuweza kusaidia kujua iwapo wanaweza kurithi mayai ya watoto wao , kwa mujibu wa ripoti.



Hatimaye waliruhusiwa kuyatumia mayai hayo, lakini tatizo jingine likazuka. Mayai hayo yangeweza kutolewa katika hospitali ya Nanjing iwapo tu kungekuwa na ithibati kuwa hospitali nyingine iko tayari kuyahifadhi.

lakini kutokanana wasiwasi wa kisheria kuhusu mayai ambayao hayajapandikizwa, ilikuwa ni vigumu kupata taasisi nyingine ya afya China iliyotaka kujihusisha.

Na kutokana na kwamba ubebaji mimba ya mtu mwingine ni haramu China, nafasi iliyosaliua ilikuwa ni kutafuta mbebaji mimba katika nchi ya nje.
Kuthibitisha uzazi na uraia

Hatimaye, babu na bibi yake mtoto huyo walishirikiana na shirika linalotafuta wanawake wanaobeba mimba za watu wengine na waliangukia eneo la Laos, ambako mpango huo unaruhusiwa kisheria.
Na huko Laos, mayai yalipandikizwa ndani ya kizazi cha mama mbebaji na ilipofika Desemba 2017 mtoto huyo wa kivulana alizaliwa.

Uraia wa mtoto huyo, aliyepewa jina Tiantian, lilikuwa ni tatizo jingine na kwa hivyo waliamua azaliwe China na sio Laos - ambapo ilibidi mwanamke huyo asafirishwe kwa viza ya kitalii.


Source: Click Here

Labels:

Wednesday, April 11, 2018

Mmiliki wa Facebook Akiri Kampuni Yake Inakabiliana na Urusi


Mmiliki wa Facebook Akiri Kampuni Yake Inakabiliana na Urusi


Mmiliki wa Facebook amewaambia maseneta wa Marekani kuwa kampuni yake imekuwa ikipambana na watumiaji wa Warusi wanaotaka kuutumia vibaya mtandao huo wa kijamii
" Haya ni makabiliano ya kijeshi. Watarekebika ,"alisema he said.
Bw Zuckerberg alikua akijibu maswali kuhusiana na sakata ya matumizi mabaya ya data za kibinafsi maarufu kama Cambridge Analytica.
Pia amefichua kuwa Robert Mueller, kutoka baraza maalum linalochunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa Mwaka 2016 aliwahoji wafanyakazi wa Facebook.

Lakini aliongeza kuwa : "kazi yetu na baraza maalum ni ya siri na ninataka kuhakikisha kwamba katika kikao cha wazi sifichui chochcote juu ya taarifa za siri.
Mwezi Februari, Ofisi ya Bw Mueller ilishtakiwa na Warusi 13 kwa kudukua taarifa za uchaguzi wa mwaka 2016, pamoja na makampuni matatu ya Urusi.
utokana na hojaji hiyo hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka mpaka kufikia asilimia nne

Kutokana na kuhojiwa kwa Bw Zuckerberg na seneti ya Marekani hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka hadi kufikia asilimia nne
Bw Zuckerberg amesema kuwa kampuni yake sasa imetengeneza nyenzo za kubaini akaunti gushi.
Awali Mtendaji mkuu wa mtandao wa kijamii Facebook, Mark Zuckerberg ameomba msamaha kwa kamati ya Seneti ya Marekani kwa kuruhusu makampuni kadhaa kutumia vibaya data binafsi za jukwaa hilo kisiasa.
Mark Zuckerberg alijitetea kwa muda wa saa tano katika jopo la wasikilizaji kutoka bunge la seneti la Marekani linalohusika na masuala ya biashara na kamati ya mahakama.

Kwamba wakati wote kutakuwa na kitengo kisicholipiwa cha Facebook, kunachoweza kulipiwa , kitengo ambacho hakina matangazo ya biashara cha mtandao wa kijamii
Kukabiliana na kauli za uchochezi wa chuki " una kiwango cha juu cha makosa kuliko vile ninavyotaka "
Binafsi alihofia juu ya uwezekano wa upendeleo wa kisiasa kwneye kampuni yake

Kinyume na matarajio ya ulimwengu, wakati wa kikao dhidi yake badala ya kuvaa fulana kama alivyozoeleka, Bw Zuckerberg alikuwa maevalia nadhifu suti nyeusi
Kutokana na hojaji hiyo hisa za mtandao wa Facebook jana ziliongezeka mpaka kufikia asilimia nne , nao wanasheria nchini Uingereza na Marekani wameanzisha mashtaka dhidi ya Facebook, Cambridge Analytica, na makampuni mengine mawili yanayounganishwa na kesi hiyo.
Na baada ya utetezi wake Mark ameelezea hisia zake kutokana na mtandao wa Facebook hapa ulipofikia na yanayojiri hafurahishwi na chochote.
Utetezi wa Mark Zuckerberg, umepokelewa vyema na masoko ya hisa na hivyo kuifaidia Facebook kwa ongezeko la hisa asilimia nne unusu.

Labels:

Wednesday, April 4, 2018

Makao Makuu ya YouTube Yavamiwa Wafanyakazi Wapigwa Risasi



Mwanaharakati mmoja wa wanyama nchini Marekani ametekeleza tukio la kisasi la kuwashambulia kwa risasi wafanyakazi wanne wa mtandao wa YouTube baada ya malalamiko yake mengi aliyokuwa akiwatumia kushindwa kufanyiwa kazi.

Nasim Aghdam, 39, has been identified as the woman who shot a man and two women with a handgun when she stormed YouTube's headquarters in San Bruno, California on Tuesday
Mwanaharakati Nasim Aghdam aliyetekeleza tukio hilo.

Mwanamke huyo aliyetambulika kwa jina la Nasim Aghdam (39) mkazi wa California Jana Aprili 04, 2018 alitembelea Ofisi za Makao makuu ya YouTube mjini San Bruno na kufyatua risasi kwa kutumia bastola ambapo baada ya tukio hilo alijiua kwa kujipiga risasi mwenyewe.

Mtandao wa Washington Post umeeleza kuwa mwanamke huyo alitekeleza shambulizi hilo baada ya kutuma malalamiko yake kwa zaidi ya mara tano kuhusu mtandao huo kuwa unanyanyasa watumiaji wake na umekuwa na sera za kidikteta.

Baadhi ya malalamiko ya Nasim kuhusu malipo ya mtandao wa YouTube


Nasima alianza kuulalamikia mtandao wa YouTube kwa kuposti mabango kwenye mitandao miingine ya kijamii akitaka watu waususie mtandao huo kutokana na sera zake za kidikteta.

Mtandao wa YouTube umethibitisha taarifa hizo ambapo ulitangaza watu wanne kujeruhiwa vibaya lakini baadaye majeruhi watatu waliaga dunia.


Tayari Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao wa YouTube, Susan Wojcicki kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa pole kwa ndugu na jamaa waliyopatwa na tatizo hilo.

Hata hivyo, mpaka sasa hakuna taarifa yoyote mbaya kutoka kwa jeshi la polisi mjini California juu ya majeruhi hao wanne.

Rais wa Marekani, Donald Trump naye kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa pole kwa wafanyakazi wa mtandao wa YouTube.

Labels:

Monday, April 2, 2018

Chombo cha Anga za Juu cha China Chaanguka Pacific

Chombo cha anga za juu cha China kilichoacha kutumika Tiangong-1 kimemeguka vipande vingi kikiingia anga ya dunia na kuanguka maeneo ya bahari kusini mwa Pacific.


Chombo hicho kiliingia anga ya dunia saa 00:15 GMT Jumatatu, idara ya anga za juu ya China imetangaza.

Tiangong-1 ilirushwa angani mwaka 2011 kufanyia majaribio teknolojia ya kuunganisha vyombo mbalimbali anga za juu na pia vyombo vya kuzunguka kwenye mzingo wa dunia.

Chombo hicho ni sehemu ya juhudi za China za kuunda kituo cha anga za juu kitakachokuwa kinadhibitiwa na binadamu katika anga za juu kufikia mwaka 2022.

Kiliacha kufanya kazi Machi 2016.

Tunayoyafahamu kuhusu eneo ambalo kilianguka?

Maafisa wanasema tu kwamba kilianguka "juu ya Pacific Kusini".

Wataalamu wa anga za juu wa Marekani wamesema wametumia teknolojia ya kufuatilia mzingo wa dunia kuthibitisha kuingia ardhini kwa Tiangong-1.

Mtaalamu wa anga za juu Jonathan McDowell kutoka Harvard ameandika kwenye Twitter kwamba huenda chombo hicho kimeanguka kaskazini magharibi mwa Tahiti.

Wataalamu walitatizika kubaini hasa ni wapi chombo hicho kingeanguka.

Idara ya anga za juu ya China ilikuwa awali imekadiria kimakosa kwamba chombo hicho kingeanguka karibu na Sao Paulo, Brazil muda mfupi kabla ya chombo hicho kuingia anga ya dunia.

Shirika la Anga za Juu la Ulaya lilisema mapema kwamba uwezekano mkubwa ni kwamba chombo hicho cha Tiangong-1 kingeanguka baharini.


ESA walisisitiza kwamba uwezekano wa mtu kugongwa na vifusi vhya vyombo hicho ulikuwa "chini ya mara milioni kumi ya uwezekano wa mtu kupigwa na radi."

Haijabainika ni kiasi gani cha vifusi hivyo kimeanguka ardhini.

Mbona chombo hiki kikaanguka hivi?
Tiangong kilifaa kusitisha shughuli yake ya kuizunguka dunia kwa utaratibu na mpangilio fulani.

Ni chombo kilichokuwa na urefu wa mita 10 (futi 32) na uzani wa zaidi ya tani 8 na ni kikubwa zaidi ya vyombo vyote vilivyoundwa na binadamu ambavyo vimewahi kuanguka kutoka anga za juu.

Lengo lilikuwa kutumia vifaa vinavyokipa chombo hicho msukumo kukielekeza hadi maeneo ya mbali yasiyo na watu maeneo ya Bahari ya Kusini.

Lakini kabla ya hilo kufanyika, ghafla mfumo wa kukidhibiti ulikumbwa na hitilafu na wataalamu wa China wakapoteza udhibiti.

Mashirika 13 ya anga za juu ya mataifa mbalimbali, yakiongozwa na Shirika la Anga za Juu la Ulaya (ESA), yalifuatilia njia ya Tiangong na kujaribu kuiga tabia yake kadiri kilivyokaribia kuingia ndani ya anga ya dunia huku kikiendelea kuizunguka.

Mwanananga Wang Yaping alitoa mhadhara unaokumbukwa sana kwa watoto akiwa moja kwa moja kutoka chombo cha Tiangong-1 kikiwa anga za juu
Chombo hiki kirirushwa mwaka 2011 kufanyia majaribio utaratibu wa kutuma vyombo vingine na kuviunganisha vikiwa anga za juu
Makundi mawili ya wanaanga yalizuru chombo hicho wakitumia vyombo vidogo kwa jina Shenzhou - mwaka 2012 na 2013
Walijumuisha wanaanga wa kwanza wa kike kutoka China Liu Yang na Wang Yaping
China inapanga kutuma chombo cha anga za juu cha kudumu katika mwongo mmoja ujao
Imeunga roketi inayobeba kuinua vitu vya uzani wa juu sana kwa jina Long March 5 kwa ajili ya kazi hiyo
Ndicho chombo kikubwa zaidi kuwahi kuanguka kutoka angani?

Tiangong ni miongoni mwa vyombo vingine vikubwa vilivyowahi kuanguka bila kudhibitiwa, lakini bado kineachwa nyuma na vyombo vingine.

Chombo cha Skylab cha Marekani kilikuwa na uzani wa tani 80 kilipoanguka, ingawa kiliweza kudhibitiwa kwa kiasi fulani, mwaka 1979.

Kilianguka Australia Magharibi ardhini lakini hakuna aliyejeruhiwa.

Chimbuko la Illuminati na dhana kuhusu nguvu zao
Chombo cha Nasa cha Columbia nacho kilikuwa na uzani wa tani 100 kilipoanguka mwaka 2003.

Tena, ardhini hakuna aliyegongwa na vifusi vyake ambavyo vilitapakaa majimbo ya Texas na Louisiana.

Mtaalamu Jonathan McDowell kutoka Kituo cha Fizikia ya Anga za Juu cha Harvard-Smithsonian anasema kwa kukadiria, 50 ni chombo cha 50 kwa ukubwa.

Mnamo 2001, Uchina ilizindua vyombo vyake vya anga kwa kujaribu kuwatuma wanyama mwaka 2003 kwenye chombo cha anga za mbali kwenye mzingo wa dunia, na hivyo kuifanya nchi hiyo kuwa ni ya tatu kufanya hivyobaada ya Muungano wa Usovieti na Marekani.

Mpango wa vituo vya safari za anga za mbali ulianza kwa kukituma chombo cha Tiangong-1 ama "Kasri la Mbinguni", mwaka 2011.

Kituo hicho kidogo kiliweza kuwahifadhi wataalam wa masuala ya anga za mbali lakini kwa muda mfupi wa siku kadhaa. Mchina wa kwanza mwanamke mtaalamu wa anga za juu Liu Yang alitembelea kituo hicho mwaka 2012.

Kilikamilisha huduma zake mwezi Machi 2016, miaka miwili zaidi ya muda kiliopangiwa.

Labels:

Thursday, March 22, 2018

Mark Zuckerberg awaomba radhi Watumiaji wa Facebook


Mwanzilishi wa Facebook na CEO Mark Zuckerberg ameibuka kwa kuomba radhi baada ya kashfa ya Cambridge Analytica kuingilia data za watumiaji million 50 wa mtandao wa Facebook.


Mark amesema kutokana na kitendo hicho kimewavunjia uaminifu na pia ameahidi kufanyika mabadiliko kadhaa ili kutoingiliwa na kuibiwa kwa taarifa za watumiaji wake.

Kupitia mtandao huo Mark ameandika:

I want to share an update on the Cambridge Analytica situation — including the steps we’ve already taken and our next steps to address this important issue.

We have a responsibility to protect your data, and if we can’t then we don’t deserve to serve you. I’ve been working to understand exactly what happened and how to make sure this doesn’t happen again. The good news is that the most important actions to prevent this from happening again today we have already taken years ago. But we also made mistakes, there’s more to do, and we need to step up and do it.

Here’s a timeline of the events:

In 2007, we launched the Facebook Platform with the vision that more apps should be social. Your calendar should be able to show your friends’ birthdays, your maps should show where your friends live, and your address book should show their pictures. To do this, we enabled people to log into apps and share who their friends were and some information about them.

In 2013, a Cambridge University researcher named Aleksandr Kogan created a personality quiz app. It was installed by around 300,000 people who shared their data as well as some of their friends’ data. Given the way our platform worked at the time this meant Kogan was able to access tens of millions of their friends’ data.

In 2014, to prevent abusive apps, we announced that we were changing the entire platform to dramatically limit the data apps could access. Most importantly, apps like Kogan’s could no longer ask for data about a person’s friends unless their friends had also authorized the app. We also required developers to get approval from us before they could request any sensitive data from people. These actions would prevent any app like Kogan’s from being able to access so much data today.

In 2015, we learned from journalists at The Guardian that Kogan had shared data from his app with Cambridge Analytica. It is against our policies for developers to share data without people’s consent, so we immediately banned Kogan’s app from our platform, and demanded that Kogan and Cambridge Analytica formally certify that they had deleted all improperly acquired data. They provided these certifications.

Last week, we learned from The Guardian, The New York Times and Channel 4 that Cambridge Analytica may not have deleted the data as they had certified. We immediately banned them from using any of our services. Cambridge Analytica claims they have already deleted the data and has agreed to a forensic audit by a firm we hired to confirm this. We’re also working with regulators as they investigate what happened.

This was a breach of trust between Kogan, Cambridge Analytica and Facebook. But it was also a breach of trust between Facebook and the people who share their data with us and expect us to protect it. We need to fix that.

In this case, we already took the most important steps a few years ago in 2014 to prevent bad actors from accessing people’s information in this way. But there’s more we need to do and I’ll outline those steps here:

First, we will investigate all apps that had access to large amounts of information before we changed our platform to dramatically reduce data access in 2014, and we will conduct a full audit of any app with suspicious activity. We will ban any developer from our platform that does not agree to a thorough audit. And if we find developers that misused personally identifiable information, we will ban them and tell everyone affected by those apps. That includes people whose data Kogan misused here as well.

Second, we will restrict developers’ data access even further to prevent other kinds of abuse. For example, we will remove developers’ access to your data if you haven’t used their app in 3 months. We will reduce the data you give an app when you sign in — to only your name, profile photo, and email address. We’ll require developers to not only get approval but also sign a contract in order to ask anyone for access to their posts or other private data. And we’ll have more changes to share in the next few days.

Third, we want to make sure you understand which apps you’ve allowed to access your data. In the next month, we will show everyone a tool at the top of your News Feed with the apps you’ve used and an easy way to revoke those apps’ permissions to your data. We already have a tool to do this in your privacy settings, and now we will put this tool at the top of your News Feed to make sure everyone sees it.

Beyond the steps we had already taken in 2014, I believe these are the next steps we must take to continue to secure our platform.

I started Facebook, and at the end of the day I’m responsible for what happens on our platform. I’m serious about doing what it takes to protect our community. While this specific issue involving Cambridge Analytica should no longer happen with new apps today, that doesn’t change what happened in the past. We will learn from this experience to secure our platform further and make our community safer for everyone going forward.

I want to thank all of you who continue to believe in our mission and work to build this community together. I know it takes longer to fix all these issues than we’d like, but I promise you we’ll work through this and build a better service over the long term.

Labels: