Sunday, July 10, 2022

Usajili wa wachezaji soka Ulaya

Hapa utaona dondoo za usajili kutoka  maeneo mbalimbali Ulaya.


Arsenal inachuana na Manchester United katika harakati za kumsajili kiungo wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante (31).



Kiungo wa Barcelona na Hispania Sergio Busquets (33) anasakwa na vilabu kadhaa vya ligi ya Marekani MLS ili kujiunga navyo msimu ujao.


Chelsea inataka £7m kutoka kwa Barcelona kwa ajili ya mlinzi wake mhispania Cesar Azpilicueta (32)  ambaye ameshakubaliana  kuhusu maslahi binafsi na klabu hiyo ya Catalan.


Arsenal na Newcastle zinamtaka kiungo mshambuliaji wa Lyon na Brazil Lucas Paqueta lakini ada ya 65m euros inayotakiwa na wafaransa hao kwa ajili ya nyota huyo mwenye miaka (24).

Arsenal iko kwenye mazungumzo na Benfica baada ya kupeleka ofa ya £6.4m kwa ajili ya kumsajili beki wa kushoto mhispania Alex Grimaldo (26).



Chelsea wanajiandaa kukubaliana na ada wanayotaka Napoli ya £34m kwa ajili ya mlinzi wake wa kati raia wa Senegal Kalidou Koulibaly (31).


Bayern Munich inamsaka mshambuliaji wa Tottenham na England Harry Kane (28) kama mbadala wa Robert Lewandowski (33) kutoka Poland anayetaka kuachana na mabingwa hao wa Bundesliga msimu huu.


Chelsea na Paris St-Germain nazo zitaingia kwenye mbio za kutaka saini ya  Lewandowski kama itashindikana kujiunga na Barcelona.


Barcelona wanaamini watamsajili kiungo mreno Bernardo Silva (27) kutoka Manchester City.


Labels:

Akpan asajiliwa Simba Sc

Kiungo wa katikati ya dimba mwenye uwezo mkubwa wa kuhimili mechi za aina zote. 

Victor Akpan ni 𝗠𝗡𝗬𝗔𝗠𝗔 🦁 #Akpan #NguvuMoja

Labels:

Saturday, July 9, 2022

Kyombo rasmi atua Simba

 HATIMAYE, Simba imepata saini ya aliyekuwa mshambuliaji wa Mbeya Kwanza, Habib Kyombo kwa mkataba wa miaka miwili baada ya kutokea sintofahamu hapo awali.

Awali nyota huyo alidaiwa kusaini timu mbili tofauti akianza na wageni wa Ligi Kuu Bara Singida Big Stars kisha kuvunja mkataba kwa makubaliano ya pande mbili baada ya kukubali dili jipya la kujiunga na Simba.


Wakati akiitumikia Mbeya Kwanza katika msimu ulioisha Juni 29, mwaka huu staa huyo alifunga mabao sita ya Ligi Kuu Bara katika mechi 15 alizocheza na kikosi hicho ambacho  kimeshuka daraja baada ya matokeo mabovu.


Huu ni usajili wa kwanza Simba kwa wachezaji wazawa msimu huu baada ya ule wa Moses Phiri raia wa Zambia aliyejiunga na miamba hiyo Juni 15 akitokea klabu ya Zanaco ya huko nchini kwao Zambia.


Mbali na Usajili huo kuna nyota wengine wanaosadikika wamejiunga na miamba hiyo ni Victor Akpan kutoka Coastal Union, Cesar Manzoki (Vipers FC), Nelson Okwa (Rivers United) na Augustine Okrah aliyetokea Asante Kotoko.


Labels:

Friday, July 8, 2022

Jack Wilshere ametangaza hivi leo kustaafu kucheza soka la kulipwa

Amestaafu kucheza soka la kulipwa akiwa na umri wa miaka 30.



Katika ukurasa wake wa twitter ameandika haya,



#soma zaidi HAPA


Labels:

Sepp Blatter na Michel Platini wafutiwa mashtaka ya ulaghai na mahakama ya Uswizi

Sepp Blatter na Michel Platini wafutiwa mashtaka ya ulaghai na mahakama ya Uswizi.

  • Wawili hao waliachiliwa huru kwa shtuma ya kufanya malipo ya faranga za Uswizi milioni 2 yaliyofanywa mwaka 2011.
  • Malipo yaliyofanywa kwa Platini kwa huduma za ushauri za Fifa.


Sepp Blatter na Michel Platini wamefutiwa mashtaka ya ulaghai katika mahakama ya Uswizi. 


Wanaume hao wawili, waliokuwa miongoni mwa vigogo wa soka, waliachiliwa huru kwa kupanga malipo ya faranga milioni mbili za Uswizi (£1.7m) kinyume cha sheria mwaka 2011. Wakati huo, Platini alikuwa rais wa Uefa na makamu wa rais wa Fifa na alitarajiwa kumrithi Blatter kama rais wa Fifa, shirikisho la soka duniani.


Malipo kwa Platini kwa huduma za ushauri katika muhula wa kwanza wa Blatter kama rais, kuanzia 1998 hadi 2002, yaliidhinishwa na Blatter Januari 2011 lakini yakaishia kumaliza kazi za wanaume katika soka.


 Waendesha mashtaka wa Uswizi walikuwa wameiambia mahakama huko Bellinzona kwamba "ilifanyika bila msingi wa kisheria" na "ilimtajirisha Platini isivyo halali" lakini hakimu katika kesi yao aliwakuta hawana hatia. Platini sasa atarejeshewa CHF 2m yake. 


Kamati ya maadili ya Fifa ilikuwa imewapiga marufuku kujihusisha na soka na kuwaondoa madarakani, na Blatter na Platini walipeleka kesi zao kwa kamati ya rufaa ya Fifa bila mafanikio na baadaye katika rufaa tofauti kwa mahakama ya usuluhishi wa masuala ya michezo.


#soma zaidi HAPA


Labels:

Thursday, July 7, 2022

Timu ya taifa Ghana yafanya usajili

Tariq Lamptey abadili utaifa kutoka Uingereza hadi Ghana.

Chama cha Soka cha Ghana kilithibitisha kuwa beki huyo wa pembeni wa Brighton, ambaye aliiwakilisha Uingereza katika mechi tofauti za vijana na kucheza mara mbili kwa Vijana wa U-21, aliamua kuchezea Black Stars.


Atakuwepo kwenye mchujo kuelekea Kombe la Dunia nchini Qatar, ambapo Ghana itamenyana na Korea Kusini, Ureno na Uruguay katika Kundi D.


"Siku zote tumeshikilia kuwa hatutajiwekea kikomo kwa kikundi kidogo tu cha wachezaji lakini tutasaka vipaji vya juu kote ulimwenguni ambao wako tayari kujitolea kwa ajili ya taifa na kutupeleka kwenye ngazi nyingine," taarifa kutoka Chama cha Soka Ghana ilisema hivyo.


Mchezaji mwingine alie amua kulitumikia taifa hilo ni Inaki Williams anaekipiga kunako Athletic Bilbao inayocheza ligi kuu ya Uhispania (LaLiga).

Labels:

Christian Eriksen kutua Man United

Mikataba sasa iko tayari kwa Christian Eriksen kusaini na Manchester Utd, kinachosubiriwa ni vipimo tu ndipo itakamilika.

Mkataba wa miaka mitatu umethibitishwa, Eriksen ndiye atakayesajiliwa na United baada ya Tyrell Malacia.

#source Twitter












Labels:

Raheem Sterling anakaribia kuhamia Chelsea


Chelsea watawasiliana moja kwa moja na Manchester City leo ili kukamilisha dili la Raheem Sterling. Ada karibu ikubaliwe pauni milioni 45 za uhakika pamoja na nyongeza, sawa na Gabriel Jesus kwa Arsenal. 


Masharti ya kibinafsi yalikubaliwa kikamilifu, Tuchel tayari alikuwa na mazungumzo ya moja kwa moja na Sterling. 

#source Twitter

Labels:

Monday, July 4, 2022

Gabriel asajiliwa Arsenal washika bunduki wa London.

Vilabu vitatu vilijaribu kupindua mkataba wa Gabriel Jesus hadi Jumapili, Juni 26… lakini kila mara alitaka Arsenal iwe kipaumbele. Sasa hatimaye ni rasmi na imethibitishwa.


Alisainiwa wiki iliyopita, ametambulishwa leo. £45m kwenda Man City. Mkataba hadi Juni 2027.

#source Twitter










Labels:

Monday, May 21, 2018

Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu ya Leo

Meneja wa Chelsea Antonio Conte

Manchester City wanampango wa kumsajili kiungo wa kati wa Chelsea Eden Hazard 27, kwa mkataba wa £100m baada ya meneja Pep Guardiola kumuweka mchezaji huyo kuwa kiungo muhimu anayemlenga wakati wa uhamisho.(Star)

Klabu ya Utaliano ya AC Milan imempatia kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini 30, mkataba wa miaka mitatu huku kiungo huyo raia wa Ubelgiji kuwa huru kwa uhamisho wa bure katika majira ya joto. (Times - subscription required)

Beki wa Tottenham,Toby Alderweireld 29, ni miongoni mwa wanaotarajiwa kuuzwa na klabu hiyo kwenda Manchester United wakati wa uhamisho wa majira ya joto. (Mirror)

West Ham inaamini kumteuwa Manuel Pellegrini kama meneja wao mpya wiki hii- ambayo itaipatia nafasi nzuri ya kumsajili kiungo wa kati Yaya Toure, 35, aliyeiaga Manchester City. (Telegraph)

Meneja wa Chelsea Antonio Conte anatarajiwa kuiaga Chelsea kwa saa 48 zijazo - huku meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique anatarajiwa kuchukua nafasi hiyo. (Express)

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere

Kiungo wa kati wa Arsenal Jack Wilshere, 26 yuko tayari kutia saini mkataba wa miaka mitatu aliyopewa na Arsenal, licha ya kupata mapendekezo bora kutoka Everton na Wolves. (Mirror)

Manchester United imekubaliana katika hatua za kwanza na kiungo wa kati kutoka Brazil Talisca, 24 ambaye amekuwa kwenye mkopo na Besiktas kutoka Benfica. (Star)

Kocha wa zamani wa Paris St-Germain Unai Emery ni miongoni mwa makocha wanaowania kukinoa kikosi cha Arsenal msimu ujao wa ligi kuu huku Mikel Arteta akiwa bado ni mmoja wa makocha anaetazamiwa kuchukua nafasi ya Arsene Wenger. (Dail Mail)

Mlinda lango kutoka Ubelgiji Thibaut Courtois

Mlinda lango kutoka Ubelgiji Thibaut Courtois 26, ametishia kuihama Chelsea iwapo klabu hiyo haitatumia pesa zake kama klabu za ''Manchester United na City'' msimu huu wa joto. (Sun)

Mazungumzo ya Napoli na meneja wao Maurizio Sarri yametibuka kutokana na matamanio ya meneja huyo kutaka kuhamia Chelsea. (Mirror)

Mhispania Santi Cazorla 33, amepewa nafasi ya kujiunga na klabu yake ya zamani ya Villarreal kuelekea kumalizika kwa mkataba wake na Arsenal. (Evening Standard)

Kiungo wa kati wa Ac Milan Suso

Kiungo wa kati wa Ac Milan Suso 24, anatarajiwa kurudi Liverpool lakini si kwa mara moja kwa siku zijazo. (Liverpool Echo)

Beki Partick Thistle Niall Keown 23, anatarajiwa kubadili majukumu yake kutoka Republic hadi Kaskazini mwa Ireland - na meneja Michael O'Neill anataka kumsajili kiungo wa kati wa Klabu ya QPR Sean Goss 22, kwa mkopo. (Daily Record)

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amefuta akaunti yake ya Instagram kutokana na matusi ambayo aliyoyapata baada ya mashetani hao wekundu kushindwa kwenye fainali ya kuwania kombe la FA dhidi ya Chelsea. (Sun)

Labels:

Wednesday, May 16, 2018

City Wamebeba Ubingwa Lakini United Watapewa Pesa Nyingi


City Wamebeba Ubingwa Lakini United Watapewa Pesa Nyingi Kuliko Wao, Sababu ni hii


Msimu wa EPL 2017/2018 umekwisha rasmi siku ya Jumapili tarehe 13/5, na mabingwa wameshapatikana ni Manchester City huku pia timu zinazoshuka daraja zimeshajulikana ni Stoke City, Swansea na West Bromwich Albion.

Kushinda kwa Manchester City kunamaanisha watapewa £153.2m kutoka EPL, pesa hizi ni kutokana na namna ambavyo mechi zao zimerushwa na pia kuna kiasi cha pesa ambacho timu zote za EPL hupewa.

Iko hivi City kama bingwa anapewa £39.8m kutoka Epl, lakini pia kuna hii pesa ambayo kila timu wanapewa kiasi sawa(equal share) ambapo huwa ni £82m, pia kuna pesa kutokana na idadi ya mechi zako zilizooneshwa live(haki kutoka Epl) na hii walitakiwa kulipwa £31.5m, jumla ya pesa zote hizi ni £153.2m.

Sasa linapokuja suala la United wao japo wamemaliza nafasi ya pili lakini watapewa pesa kuliko bingwa, United watapokea £153.6 kwanini? Baasi ni hivi United wanapokea kama kawaida equal share ya £82m, wakati City anapokea £39.8m za ubingwa, United wanapokea £37.8m ya mshindi wa pili, lakini United mechi zao ambazo EPL walirusha hewani live ni mechi mbili zaidi ya City na hii imewapa £33.9m katika mechi hizo na hapa ndipo walipowaacha City.

Suala hili lipo pia kwa mshindi wa 3 na wa 4, Tottenham amemaliza ligi katika nafasi ya 3 lakini jumla ya pesa ambayo wamevuna ni kiasi cha £148.1m, hii ni pesa ndogo kuliko ambayo Liverpool ambao wamemaliza ligi katika nafasi ya 4 wamevuna, Liverpool wamepata £149.6m na hii ni kutokana na mechi zilizoenda live.

Vilabu vilivyoshuka daraja navyo sii haba kwani wameshuka na fungu kubwa la pesa, Swansea amevuna £100m, West Bromich wakiweka mfukoni kiasi cha £98.5m sawa na mshindi wa mwisho Stoke City na hii imechagizwa sana na hii pesa £82.0m ambayo EPL wamekuwa wakitoa kwa kila timu.

Labels:

Mechi 7 Bila Ushindi Yanga imepotea Wapi!!


Yanga imecheza mechi saba bila ushindi katika mashindano yote inayoshiriki (ligi kuu Tanzania bara na Caf Confederation Cup).

Mechi sita ambazo Yanga haijashinda ni Wolaitta Dicha 1-0 Yanga, Mbeya City 1-1 Yanga, Yanga 1-1 Singida, Simba 1-0 Yanga, USM Alger 4-0 Yanga, Tanzania Prisons 2-0 Yanga na Mtibwa Sugar 1-0 Yanga.

Juzi Jumapili Mei 13, 2018 Yanga ilikuwa ugenini ikicheza na Mtibwa Sugar kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro ambapo wamepoteza mchezo huo kwa kufugwa goli 1-0.

Baada ya kufungwa 2-0 na Tanzania Prisons kwenye mechi iliyopita, Yanga imepoteza mchezo wa pili mfululizo kufuatia kipigo hicho.

Hadi sasa Yanga imepoteza mechi nne za ligi baada ya kucheza mechi 26 huku ikiwa na mechi mbili mkononi (viporo). Mechi zote ambazo Yanga imepoteza ilicheza ugenini (Mbao 2-0 Yanga, Simba 1-0 Yanga, Tanzania Prisons 2-0, Mtibwa Sugar 1-0 Yanga).

Imepoteza mechi tatu mfululizo kati ya nne, Simba 1-0 Yanga, Tanzania Prisons 2-0 Yanga, Mtibwa Sugar 1-0 Yanga. Katika mechi hizo, Yanga haijafanikiwa kufunga goli hata moja.

Yanga inaendelea kubaki nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 48 nyuma ya Azam (pointi 52) na Simba (pointi 68). Ushindi dhidi ya Yanga unaifanya Mtibwa Sugar ifikishe pointi 37 na kukaa katika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi.

Labels:

Tuesday, May 15, 2018

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne ya Leo




Kiungo wa kati wa Newcastle Jonjo Shelvey, 26, hatajumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kitakachoshiriki kombe la dunia kutokana rekodi yake mbaya kinidhamu. (Mirror)

Manchester United wako tayari kuilipa Napoli pauni milioni 44 kumpata beki Elseid Hysaj msimu huu. Raia huyo wa Albania wa umri wa miaka 24 atakuwa mlinzi namba saba ghali zaidi duniani. (Sun)

Everton watamfuta meneja Sam Allardyce saa 48 zinazokuja na wanakaribia kumteua aliyekuwa meneja wa Watford Marco Silva. (Mirror)

Afisa mkuu mtendaji wa Arsenal Ivan Gazidis na mkurugenzi mkuu Josh Kroenke wamemtambua kiungo wa kati wa zamani wa Arsenal Mikel Arteta ambaye sasa ni kocha huko Manchester City kama mtu anayeweza kuchukua mahala pake Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Mail)

Meneja wa Juventus Massimiliano Allegri bado anaweza kuwa meneja wa Arsenal ikiwa atashinda vita vya kuhama wachezaji. (Star)

Mshambulizi wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang anasema alijiunga na klabu hiyo akiwa na imani kuwa Wenger atakabaki kama meneja kwa miaka kadhaa. (Evening Standard)

Steve Bould atachelewesha uamuzi ikiwa atabakia au la kama kaimu meneja wa Arsenal, anaposubiri kujua ni nani atakuwa meneja. (Telegraph)

West Ham walikutana na meneja wa Shakhtar Donetsk Paulo Fonseca saa chache baada ya mkataba wa meneja David Moyes kufika mwisho. (Mail)

West Ham watamfuta Moyes na watakuwa na majina matatu kwenye orodha yao. (Teamtalk)

Manchester City wanalenga kumsaini wing'a wa Crystal Palace na Ivory Coast Wilfried Zaha, 25. (Star)

Manchester United wanakumbwa na upinzani kutoka kwa Paris St-Geraon kumsania kiungo wa kati wa Shakhtar Donetsk Fred, 25. (Manchester Evening News)

Meneja wa Newcastle Rafael Benitez anasema hana nia ya kurejea Napoli kwa kuwa yuko kwenye mazungumzo na Magpie kuhusu mkataba mpya. (Calcio Napoli 24 - in Italian)

Benitez amefanya mazungumzo na kipa wa Paris St-Germain Alphonse Areola, 29. (France Football - via Metro)

Real Madrid wako tayari kumwendea kipa Chelsea Thibaut Courtois, 26, wakati mbelgiji huyo akiingia miezi 12 ya mwisho ya mkataba wake.

Southampton wanataka kumsaini winga wa Celta Vigo Pione Sisto, 23. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark ana kipengee cha pauni milioni 36 cha kuondoka mapema kwenye mkataba wake.

Winga raia wa Morocco Sofiane Boufal, 24, amezungumzia nia yake ya kurejea ligi ya Ufaransa siku moja tu baada ya kukamilika kwa Premier League.(SFR Sport)

Labels:

Neymar awekwa kikosi cha Brazil cha Kombe la Dunia licha ya jeraha




Brazil wamemtaka mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar, ambaye bado anauguza jeraha, katika kikosi cha wachezaji 23 ambao wanatarajiwa kuchezea taifa hilo katika michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi.

Neymar, 26, alifanyiwa upasuaji mwezi Machi na daktari wa timu ya taifa ya Brazil alisema hataweza kucheza kwa miezi mitatu.

Wachezaji wanne wanaochezea Manchester City Ederson, Danilo, Fernandinho na Gabriel Jesus ni miongoni mwa wachezaji wanaosakatia gozi Ligi ya Premia ambao wamo kwenye kikosi hicho.

Wengine ni nyota wa Liverpool Roberto Firmino na winga wa Chelsea Willian.

Beki wa kulia wa PSG Dani Alves atakosa michuano hiyo baada ya kupata jeraha la goti wiki iliyopita.


Brazil wamo Kundi E na Costa Rica, Serbia na Uswizi na watacheza mechi yao ya kwanza Jumapili 17 Juni.

Kikosi kamili cha Brazil:

Walinda lango: Alisson (Roma), Ederson (Manchester City), Cassio (Corinthians).

Mabeki: Danilo (Manchester City), Fagner (Corinthians), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atletico Madrid), Thiago Silva, Marquinhos (both PSG), Miranda (Inter Milan), Pedro Geromel (Gremio).

Viungo wa kati: Casemiro (Real Madrid), Fernandinho (Manchester City), Paulinho (Barcelona), Fred (Shakhtar Donetsk), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Barcelona), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Juventus).

Washambuliaji: Neymar (PSG), Taison (Shakhtar Donetsk), Gabriel Jesus (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool).

Labels:

Friday, May 11, 2018

Haji Manara Akataa Kuitwa Msemaji wa Simba


Haji Manara Akataa Kuitwa Msemaji wa Simba " Niite Msemaji wa Mabingwa wa Nchi"



Alhamisi ya May 10 2018 Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara club ya Dar es Salaam Young Africans walikuwa Sokoine Mbeya kucheza mchezo wao wa 25 wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Yanga wakiwa Mbeya wamekubali kupoteza mchezo mbele ya Tanzania Prisons kwa magoli 2-0, hivyo kipigo hicho kimeifanya Simba kutangazwa Bingwa wa VPL msimu wa 2017/2018 wakiwa na point 65 na michezo mitatu mkononi.


Labels:

Tanzania Prisons Yawafanyia Mbaya Yanga Yawavua Ubingwa Peupe




Mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara klabu ya Yanga imekubali kipigo cha mabao 2 – 0 dhidi ya TZ Prisons kwenye dimba la Sokoine jijini Mbeya.

Kukubali kipigo cha mabao hayo 2 – 0 dhidi ya TZ Prisons kinaifanya Yanga kuvuliwa ubingwa rasmi wa ligi kuu Tanzania Bara.

Yanga yenye pointi 48 ilihitaji kushinda michezo yote sita huku akiiyombea dua baya hasimu wake Simba kupoteza walau mechi moja ili kujihakikishia kutwaa ubingwa huo kwa mara ya nne mfululizo lakini hali imekuwa tofauti hii leo baada ya kukubali kipigo hicho mbele ya Prisons.

Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba mpaka sasa inajumla ya pointi 65 huku ikisaliwa na michezo mitatu mkononi kabla ya kumaliza msimu huu wa mwaka 2017/18.

Waliopeleka kilio mitaa ya Jangwani hii leo ni wachezaji, Eliuter Mpepo katika dakika ya 58 na Salum Bosco kunako dakika ya 85 ya mchezo.

Labels:

Samatta Aikoa Timu Yake na Kipigo Atandika Goli Moja




Kikosi cha KRC Genk jana anachocheza Mtanzania, Mbwana Samatta, jana kilikwenda sare ya bao 1-1 dhidi ya KAA Gent katika mchezo wa Play Offs kwenye ligi ya Ubelgiji.

Samatta aliingia Uwanjani dakika ya 54 ya mchezo akitokea benchi kuchukua nafasi ya Mgiriki Nikolaos Karelis wakati timu yake ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Baada ya Samatta kuingia Uwanjani, ilimchukua takribani dakika 12 kuisawazishia Genk katika dakika ya 66 ya mchezo na mechi hiyo mpaka inamalizika matokeo yalikuwa ni 1-1.

Labels:

Tuesday, May 8, 2018

Refa Atakayecheza Fainali ya Real Madrid na Liverpool Huyu Hapa




Mchezo ambao unasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka duniani kwa sasa ni fainali ya klabu bingwa barani Ulaya ambayo itawakutanisha Real Madrid na Liverpool Jumamosi ya Mei 26 mwaka huu.

Tayari kamati ya waamuzi ya UEFA imemchagua mwamuzi wa kati ambaye anachezesha mchezo huo utakaopigwa kwenye uwanja wa NSC Olimpiyskiy, Kyiv kwa kusimamia sheria 17 za soka.

Kamati hiyo imemteua Milorad Mažić kutoka nchini Serbia kuchezesha fainali hiyo ambayo inataajiwa kuwa na upinzani mkubwa kwa timu zote mbili.

Mažić, 45, amekuwa mwamuzi wa kimataifa tangu 2009 na amewahi kuchezsha fainali kadhaa ikiwemo ile ya mabara mwaka jana iliyowakutanisha Chile and Germany, UEFA Super Cup 2016 kati ya Real Madrid na Sevilla.

Labels:

Meneja mpya wa Arsenal kujulikana kabla ya kombe la dunia

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Arsene Wenger atahitimisha miaka 22 ya kuiongoza Arsenal Mei 13


Klabu ya soka ya Arsenal inauhakika wa kumtangaza meneja mpya wa timu hiyo atakayechukua mikoba ya Arsene Wenger, kabla ya kuanza kwa fainali za michuano ya kombe la dunia.

Washika mitutu hao wa London,hawajaweka hadharani lini itakuwa muda rasmi wa mwisho wa kusaka meneja mpya, lakini meneja mpya atajulikana kabla ya tarehe 14 Juni , tarehe ambayo michuano ya kombe la dunia itakuwa inaanza kutimua vumbi huko nchini Urusi.

Wenger aliyedumu katika klabu ya Arsenal kwa miaka 22, ataingoza timu hiyo katika michezo miwili iliyosalia kabla ya kumalizika kwa ligi jumapili ya Mei 13.

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique

Meneja wa zamani wa Fc Barcelona Luis Enrique, anatajwa kuwa miongoni makocha wanaopewa nafasi kubwa ya kuchukua kazi za kuinoa Arsenal pia yupo meneja wa Juventus Massimiliano Allegri.

Pia viungo wawili wa zamani wa klabu hiyo Mikel Arteta ambae kwa sasa ni Kocha msaidizi wa Manchester City na Patrick Viera, anayekinoa kikosi cha New York City, pia wanapigiwa chapuo ya kupewa kazi hiyo.

Makocha wengine anaotajwa sana kuweza kuinoa Arsenal ni kocha wa Monaco Leonardo Jardim na Carlo Ancelotti.

Labels:

Tetesi za Soka Ulaya Jumanne ya Leo

Image caption Meneja wa Hudderfield David Wagner

Leicester inamtaka meneja wa Hudderfield David Wagner kuwa mkufunzi wao mpya , Foxes wanatarajia kumuaga meneja wao Claude Puel mwezi huu. (Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard ,27, amesema ''hana nafasi'' ya kuondoka Stamford Bridge kuelekea Manchester United. (Mail)


Mshambuliaji wa Chelsea na Uhispania Alvaro Morata , 25, ana uwezekano wa kurudi Juventus na Chelsea wanaweza kufikiria uhamisho wa mshambuliaji wa Paris St-Germain na Uruguay Edinson Cavani , 31. (Tuttosport, via Metro)

Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Meneja wa zamani wa Barcelona Luis Enrique anatarajiwa kuwa mkufunzi mpya wa Arsenal

Arsenal inamtaka meneja wa Juventus Massimiliano Allegri au kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique kuwa mkufunzi wao mpya, lakini wawili hao bado wanawasiwasi kuhusiana na uongozi wa klabu hiyo. (Sky Sports)

Enrique yuko katika hali ya kutaka kiwango kikubwa cha malipo yake iwapo atakuwa meneja mpya wa Arsenal- baada ya kutaka kulipwa £15m baada ya kukatwa ushuru. (Mirror)

Meneja wa Napoli Maurizio Sarri ambaye amehusishwa na Chelsea ametoa pendekezo la kuiaga upande wa klabu hiyo ya Serie A wakati wa majira ya joto iwapo atadhibitisha kuna kifungu cha kutolewa kwa yuro milioni 8 katika mkataba wake. (Talksport)

Liverpool imezungumza na Juventus kuhusu mkataba wa Sami Khedira mwenye umri wa miaka 31 wakati wa uhamisho wa bure kwa kiungo wenzake Mjerumani Emre Can, 24, kuelekea upande wa Italia. (Sun)

Bayern Munich wako tayari kumuuza mshambuliaji raia wa Poland Robert Lewandowski, 29, anayetegewa na Manchester United. (Calciomercato, via Express)Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Kiungo wa kati wa Barcelona Andres Iniesta

Kiungo wa kati wa Barcelona Andres Iniesta pendekezo lake la uhamisho kuelekea kwenye Ligi Kuu ya Uchina inaweza kuwa na shaka baada ya Chongqing Lifan kudokeza mkataba wa Mhispania huyo mwenye umri wa miaka 33 unaweza kusitishwa kutokana na matatizo ya kifedha. (Goal.com)

Kiungo wa kati wa Wolves Ruben Neves anatarajia kuichezea klabu hiyo kwenye msimu ujao wa Ligi kuu ya Uingereza licha ya mitizamo tofauti kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 wa kimataifa. (Guardian)

Mlinda lango wa Uhispania Iker Casillas, 36, anaweza kusalia na klabu ya Porto kwa msimu mwengine baada ya kushinda taji lake la kwanza na klabu ya Ureno msimu huu. (Marca)

Mkufunzi wa Southampton Mark Highes anazidi kupata uugwaji mkono na wachezaji katika uwanja wa St Mary kuendelea kuiongoza klabu hiyo licha ya kuwa katika kiwango cha hatua ya kushushwa daraja mwishoni mwa msimu huu. (Telegraph)


Mmiliki wa klabu ya Bristol City Stephen Lansdown amesema hana ufahamu wowote iwapo mkufunzi wa klabu hiyo Lee Johnson amehusishwa na klabu ya West Brom. (Birmingham Mail)  Haki miliki ya picha REUTERS Image caption Mshambuliaji wa Manchester United na Ubeligiji Romelu Lukaku

Mshambuliaji wa Manchester United na Ubeligiji Romelu Lukaku , 24, amesema jeraha lake la kifundo cha mguu linaendelea vizuri ''kinyume na matarajio yake.'' (Manchester Evening News)

Tiketi za mechi kati ya Huddersfield dhidi ya Arsenal, ambayo ni mechi ya mwisho ya Arsene Wenger kwa the Gunners , zinauzwa kwa zaidi ya £200- licha ya onyo kwa mashabiki ''kunyanyaswa.'' (Huddersfield Daily Examiner)

Meneja wa Brighton Chris Hughton anatarajia uhamisho mwenye utaratibu kuliko wa msimu uliopita wa majira ya joto ambapo wachezaji saba walisajiliwa - sasa klabu hiyo imedhibiti wadfa yake kwenye ligi kuu Uingereza. (Argus)

Labels: