Friday, July 8, 2022

CAG Kichere naye alia na Tume ya uchaguzi ifumuliwe

Aungana na viongozi wengine, wakiwemo wastaafu, wanaotaka tume ya uchaguzi iwe na watendaji walio huru ili iweze kuaminika.

Dar es Salaam. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Charles Kichere ameishauri Serikali kuipa nguvu Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuajiri watumishi wake watakaoweza kusimamia uchaguzi kwa haki badala ya kuendelea kutegemea waliopo kwenye mfumo wa Serikali.

Mei 10, 2019, Mahakama Kuu ilitoa hukumu ya kubatilisha vifungu vya 7(1) na 7(3) vya sheria ya uchaguzi vinavyowapa mamlaka wakurugenzi wa miji, wilaya, manispaa na majiji kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye maeneo yao.

Shauri hilo lilifunguliwa na mwanaharakati wa Katiba, Bob Wangwe akishirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC).

Hata hivyo, Serikali ilikata rufaa kuipinga hukumu huyo na baadaye Oktoba 2019 Mahakama ya Rufani ikabatilisha uamuzi na hivyo kuruhusu wakurugenzi waendelee kusimamia uchaguzi.

#soma zaidi HAPA











Labels:

Thursday, July 7, 2022

Taarifa kwa UMMA kuhusu ajira ya Sensa

Taarifa kwa umma kuhusu sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.

Ofisi ya Taifa ya Takwimu imetoa tangazo hili na kulitolea ufafanuzi. Soma zaidi HAPA


Pia Kamisaa wa Sensa Anna Makinda, amesema baadhi ya Watanzania wanapenda uongo kutokana na maneno ya uzushi yanayozagaa mitandaoni kwamba majina ya wasimamizi wa Sensa hayatoki kwa sababu wameweka watoto wao, na kusema majina yakitoka waombaji wote wenye sifa watachukuliwa.


Labels:

DC Kigoma aagiza uchunguzi ujenzi wa Zahanati

Mkuu wa wilaya ya Kigoma Ester Mahawe ameagiza mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoani Kigoma, kufanya uchunguzi katika mradi wa Zahanati ya kijiji cha Samwa kata ya Kidakhwe wilayani Kigoma kufuatia mradi huo kutumia gharama kubwa na kupitiliza muda wa utekelezaji.




Agizo hilo amelitoa baada ya kamati ya siasa chama cha mapinduzi wilaya ya kigoma kufanya ziara kijijini hapo, ambapo wananchi wamelalamika mradi huo kushidwa kukamilika kwa wakati licha ya kuendelea kukosa huduma za matibabu karibu.

Awali kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Kigoma Erasto Kitabi alieleza mradi huo kusuasua kutokana na mkandarasi anayesimamia kutokuwa na uhusiano mzuri na kamati ya ujenzi licha ya kupewa fedha zote za mradi kiasi cha shilingi milioni 70.

#source Eatv










Labels:

Waziri Mkuu Uingereza ajiuzulu

 Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative.


London. Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson amejiuzulu nafasi ya kiongozi wa Chama cha Conservative.


Boris amejiuzulu nafasi hiyo leo Alhamisi Julai 7, 2022 lakini bado atabaki kuwa Waziri Mkuu mapaka chama hicho kitakapopata kiongozi mpya mwezi Oktoba.


Katika hotuba yake, Boris amesema “Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani. Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani,’’


"Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’’


 Amejiuzulu baada ya kuhudumu katika wadhifa huo chini ya miaka mitatu, licha ya kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa 2019. 


Kinachofuatia baada ya kiongozi huyo wa Conservative kujiuzulu, uchaguzi wa kiongozi mpya wa chama unaanzishwa ambapo chini ya sheria za sasa, wagombea wanahitaji kuungwa mkono na wabunge wanane wa chama hicho ili kuwania. 


#Soma zaidi HAPA










Labels:

Monday, May 21, 2018

Trump Ataka FBI Kufanyiwa Uchunguzi




Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa anahitaji uchunguzi kufanyika ilikubaini kama shirika la upelelezi la FBI lilijipenyeza kuchunguza kampeni zake kwa maslahi ya kisiasa.

Kupitia ukurasa wake wa tweeter,Trump amesema kuwa anahitaji kujua kama mtangulizi wake aliagiza kitu kama hicho kufanyika.

Katika ombi ambalo siku ya jumatatu Trump alilitoa rasmi, linakuja kufuatia baada ya vyombo vya habari vya Marekani kudai kuwa FBI walikuwa na watu wao wa siri kwenye mikutano ya ndani ya Trump kwa lengo la kumchunguza.

Hadi sasa tayari kuna taarifa za kina za kiuchunguzi kuhusiana na mwenendo mzima wa kampeni zilivyoendeshwa.

Kwa siku ya jumapili Trump kupitia ukurasa wake wa Twitter alikuwa na mfululizo wa madai ya kukanusha na kudai hakuna ushahidi wowote wa kuzihusisha kampeni zake na Urusi.

Na ni kufuatia uchunguzi unaoendelea chini ya Robert Mueller kuhusiana na jitihada za Urusi kuingilia uchaguzi wa mwaka 2016,kwa lengo la kuchagiza ushindi wa bwana Trump.

Gazeti la New York Times lilichapisha taarifa iliyodai kuwa FBI walituma mtu wao kufuatilia mwenendo wa kampeni za Trump mara tu walipopata taarifa za uwezekano wa Urusi kuingilia uchaguzi huo.

Hata hivyo vyombo vya kisheria vimegoma kutoa ushahidi majina ya maofisa waliohusika katika uchunguzi huo kwa kuhofia usalama wao.

Jambo jingine linalotarajiwa ni Trump kuagiza idara ya sheria ambayo inamvutano na FBI ili iweze kutoa nyaraka hizo za uchunguzi.

Mchambuzi wa BBC Antony Zurcher, anasema kuwa Robert Mueller anaonekana kupiga hatua katika uchunguzi wake,jambo ambalo lina muudhi Trump.

Labels:

Wednesday, May 16, 2018

Mizengo Pinda Atoa Ushauri Kuhusu Tanzania ya Viwanda



Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Kayanza Peter Pinda amezitaka taasisi za elimu na mafunzo kuhakikisha mageuzi ya kiuchumi yanafanyika nchini kwa kutoa elimu.

Mhe. Pinda ametoa ushauri huo jijini Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa Kituo cha Taaluma kuhusu nchi ya China kijulikanacho kama Centre for Chinese Studies yaani CCS, kituo ambacho ni sehemu ya taasisi za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mh. Pinda amesema mageuzi ya kiuchumi hususani kupitia ukuaji wa sekta ya viwanda, yanahitaji kuwa na jamii inayopenda kufanya kazi kwa bidii na iliyo tayari kubadilika kifikra.

Uzinduzi wa kituo hicho umefanywa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga, ambaye amesema Tanzania ina uhusiano mzuri na nchi ya China lakini inasikitisha kuona kwamba bado kama nchi haijatumia ipasavyo fursa ambazo taifa la China imezitoa kwa Tanzania.

Aidha kituo hicho kilichozinduliwa kimeelezewa kuwa jukumu lake ni kukuza uhusiano kati ya China na Tanzania pamoja na kutumia mafanikio iliyoyapata nchi ya China kwa ajili ya kuharakisha mageuzi ya kiuchumi.

Labels:

Maalim Seif Aitaka Serikali Isamehe Baadhi ya Kodi


Maalim Seif Aitaka Serikali Isamehe Baadhi ya Kodi Katika Kipindi Hiki cha Ramadhani


Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka serikali iliyopo madarakani visiwani Zanzibar inayoongozwa na Dkt. Ali Mohamed Shein iwahurumie wananchi hasa katika kipindi cha mfungo wa mwezi wa Ramadhani.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za CUF  mjini Zanzibar, amesema kuwa waliopo madarakani wasiwe hodari kuwataka wafanyabiashara wasipandishe bei za bidhaa wanazouza lakini na wao kodi ambazo hazina tija, zinawakamua wananchi waweze kuzipunguza.

"Ni vyema kujifunza kwa serikali ya Kenya ambayo imeweza kuondoa kodi kwa wafanyabiashara wale wote ambao watafanya biashara ya tende katika Mwezi wa Ramadhani", amesema Maalim Seif.

Aidha, Maalim Seif amewataka wananchi kufanya mambo ya kheri katika mwezi huo na kuacha kulumbana, kutoleana maneno yasiyofaa kwani mwezi huo ni mwezi wa rehema hivyo ni vyema kufanya mambo ya kheri yanayompendeza Mungu.

"Ni vyema kupendana,kusaidiana, kuhurumiana,kuacha kugombana na kutohasimiana ili kupata fadhila za Mwezi Mungu", amesisitiza Maalim Seif.

Kwa upande mwingine, Maalim Seif amewataka wafanyabiashara wasiuchukulie kwamba mwezi wa Ramadhani kama ni msimu wa kupata faida ya kupindukia na badala yake wauchukulie ni mwezi wa kuchuma thawabu kwa lengo la kuwasaidia wananchi hasa masikini.

Labels:

Tuesday, May 15, 2018

Watu 52 wafariki Marekani ikifungua ubalozi mpya Jerusalem



Raia 52 wa Palestina wameuawa na wengine 2,400 wamejeruhiwa na wanajeshi wa Israeli katika mapigano mabaya kuwahi kushuhudiwa tangu mwaka 2014 katika mpaka wa Gaza, maafisa wa Palestina wanasema.

Raia wa Palestina wamekuwa wakiandamana kwa wiki kadhaa lakini zimechacha leo wakati ubalozi mpya wa Marekani umefunguliwa mjini Jerusalem hatua iliyowaghadhabisha Wapalestina.

Wanaitazama hatua hiyo kama Marekani kuunga mkono utawala wa Israel katika mji huo mzima wakati wapalestina wanadai haki ya umiliki wa eneo la mashariki mwa mji huo.

Maafisa wa vyeo vya juu kutoka Marekani watahudhuria sherehe hiyo leo akiwemo binti ya Rais wa Marekani Donald Trump Ivanka na mumewe Jared Kushner.

Wengi wa maafisa kutoka Muungano wa Ulaya hawatahudhuria.

Uamuzi wa Trump wa kuhamisha ubalozi huo kutoka Tel Aviv umegadhabisha Wapalestina ambao wanadai eneo la Jerusalem Mashariki ni mji wao mku wa badaye.

Israel ilichukua udhibiti wa eneo la Jurusalem mashariki mwaka 1967 wakati wa vita vya Mashariki ya kati, na inautaja mji huo kuwa wake na usiogawanywa.




Hatua hiyo ya Trump ya mwaka uliopita ya kuutambua mji wa Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel ilivunja msimamo wa wastani wa Marekani kwa suala la mji huo na kwenda kinyume na misimamo ya nchi zingine duniani.


Ubalozi wao mdogo ulianza kutoa huduma kuanzia jana Jumatatu kwenye jengo la ofisi za ubalozi mjini Jerusalem.

Eneo lingine kubwa litatafutwa baadaye wakati ubalozi wote utahama kutoka mji wa Tel Aviv.

Sherehe za ufunguzi zilifanywa mapema ili ziweze kuenda sambamba na sherehe za miaka 70 za kuanzishwa taifa la Israel.

Rais Trump anatarajiwa kuhutubia wale ambao watahudhuria sherehe hiyo kwa njia ya video.



Kando na Ivanka Trump na Jared Kushner ambao wote ni washauri wakuu kwenye Ikulu ya White House, Waziri wa fedha wa Marekani Steven Mnuchin na naibu waziri wa mashauri ya nchi za kigeni John Sullivan watakuwa kwenye sherehe hiyo.

Muungano wa Ulaya umepinga vikali kuhamishwa kwa ubalozi huo na mabalozi wengine wa nchi za EU hawatahudhuria sherehe hiyo.

Hata hivyo wanadiplomasia kadhaa wa kigeni wanatarajiwa kuhudhuria wakiwemo waakilishi kutoka Hungary, Romania na Jamhuri ya Czech ambayo ilizuia taarifa ya pamoja ya EU kuhusu suala hilo.

Marais wa Guatemala na Paraguay pia nao wanatarajiwa kuhudhuria; nchi hizo zote mbili ziliamua kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem baada ya Trump kutoa tangazo hilo.



Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alitoa wito kwa nchi zote kujiunga na Marekani na kuhamisha balozi zao kwenda Jerusalem.

Rais wa Mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas ameutaja uamuzi wa Trump kama dafrao ya karne.


Maelfu ya Wapalestina wanakusanyika kuandamana kwenye ua unaotenganisha Israel na ukanda wa Gaza.

Muda wa kuhamishwa ubalozi huo umezua wasi wasi wa kuongezeka msukosuko huko Gaza


Tangu mwisho wa mwezi Machi zaidi ya wapalestina 40 wameuawa na wanajeshi wa Israel wakati wa maandamano ya mpakani.

Mkuu wa shurika la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa ameilaumu Israel kwa kutumia nguvu nyingi.

Hali ya mji wa Jerusalem ndiyo chanzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina.

Tangu mwaka 1967 Israel ilijenga makao mengine kwa karibu wayahudi 200,000 huko Jerusalem mashariki. Makao hayo yanatajwa kuwa haramu chini ya sheria ya kimataifa, licha ya Israel kupinga hilo.

Labels:

Friday, May 11, 2018

Mbunge Sugu: Nilifungwa Kiholela na Nimetoka Kiholela




Saa chache baada ya kutoka jela, mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu amesema ni mfungwa wa kisiasa, “nilifungwa kiholela na nimetoka kiholela.”

Viongozi wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe jana Mei 10, 2018 walifika katika Gereza Kuu la Ruanda mkoani Mbeya kuwapokea Sugu na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga lakini walipigwa chenga ya mwili baada ya kuelezwa na askari magereza kwamba wameshatoka, hivyo kulazimika kuwafuata nyumbani.

Akizungumza na MCL Digital jana Sugu amesema, “Sikutaka kuhoji sababu za kutolewa, jana niliambiwa jiandae kesho (jana) tutatoka, basi nasi tukasema haina shida kwa sababu sikuwa na sababu ya kuwa ndani. Naamini sikutakiwa kuwa gerezani.”

Sugu akiwa na Masonga alifika nyumbani kwake na kumkuta mlinzi pekee kutokana na mkewe Happiness Msonge kwenda Gereza la Ruanda kuwapokea.

Dakika chache baadaye Happiness na mke wa Masonga, Grace Malya walifika nyumbani hapo na kuwalaki kwa furaha huku wakikumbatiana na kucheka.

Akizungumzia mazingira ya kuachiwa kwa wawili hao, Mbowe amesema, “inaonyesha hawakuwa na sababu ya kuwepo gerezani maana mazingira ya kutolewa kwao ni tata sana.”

Labels:

Jeshi la Magereza: Sugu Ametoka kwa Msamaha wa Rais




Jeshi la Magereza limesema mbunge wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi maarufu Sugu ametoka kwa msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa kwa wafungwa katika maadhimisho ya miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Aprili 26, 2018.

Akizungumza na MCL Digital jana Alhamisi Mei 10, 2018, ofisa habari wa jeshi hilo, Mratibu Msaidizi wa Magereza, Lucas Mboje amesema katika maadhimisho hayo, Rais Magufuli alitoa msamaha kwa wafungwa 3,319, kati yao wafungwa 585 waliachiliwa huru Aprili 26, 2018.

“Wafungwa 2,734 walibakia gerezani akiwemo Sugu kumalizia sehemu ya kifungo kilichobakia baada ya kupewa msamaha huo na Rais Magufuli,” amesema.

Labels:

Tuesday, May 8, 2018

Kampuni ya Maxmalipo yatangaza kupunguza wafanyakazi




Kutokana na mabadiliko ya teknolojia kampuni ya Maxcom Africa imetangaza kuajiri wafanyakazi wapya wenye ujuzi unaohitajika.

Kutokana mabadiliko hayo, baadhi ya wafanyakazi waliopo ambao ama nafasi zao zitakufa kutokana na teknolojia mpya inayotumiwa na kampuni hiyo au zitakuwa zinajirudia hivyo kuilazimu kuwapunguza.

Msemaji wa Maxcom Africa, Deogratius Lazari amesema kwa sasa kampuni hiyo ina watumishi 451 lakini baada ya Serikali kuanza kutumia mfumo wa kielektroniki kwenye masuala mengi mfano utoaji wa zabuni, ukusanyaji wa mapato na maeneo mengine, baadhi ya majukumu yamepungua huku mengine yakizaliwa.

“Huwezi kurundika wafanyakazi wengi kwenye eneo moja bila kujali tija yao. Tulipunguza baadhi ya wafanyakazi walioonekana ufanisi wao upo chini mwaka jana ila awamu hii ni kutokana na mabadiliko ya teknolojia,” amesema Lazari.

Amesema yapo maeneo kadhaa ya operesheni za kampuni hiyo ambayo yameimarishwa kiteknolojia kurahisisha majukumu ya menejimenti, wafanyakazi na mawakala zaidi ya 15,000 waliopo nchini kote.

Taarifa ya uwezekano wa kupunguza wafanyakazi wake iliyotolewa na mkurugenzi wa uendeshaji wa kampuni hiyo, Charles Natai inasema utaratibu wa kisheria utazingatiwa kufanikisha mchakato huo kwa wafanyakazi watakaolazimika kupunguzwa. Taarifa ilitolewa Mei 4.

“Jambo hili linatufanya sisi kufanya uamuzi wa kupitia upya mfumo wa uendeshaji wetu na kuboresha miundombinu ya shirika ili kufikia mahitaji yetu ya kibiashara wakati tukiimarisha ufanisi,” inasomeka sehemu ya taarifa hiyo.

Labels:

Monday, May 7, 2018

Rais JPM Awapa Onyo Kali Wanachuo wa SUA "Sitosita Kuwafukuza Wote''




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, amesema hatosita kufukuza wanafunzi wa chuo watakaobainika kufanya vurugu shuleni na kuacha kuzingatia masomo, na suala hilo sio vitisho bali ni ukweli mtupu.


Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye ziara yake Chuo Kikuu cha Kilimo cha SOkoine (SUA) mkoani Morogoro, na kuwataka wanafunzi wote vyuoni kuzingatia masomo yao, na sio kujihusisha na vurugu hasa za kisiasa, kwani akigundua hilo atafukuza wote hata kama ni chuo kizima, na iwapo atafanya hivyo, hajui kama atawarudisha tena chuoni.

"Niwaombe ndugu zangu, mmekuja hapa kwa ajili ya shule, msipoteze muda wenu kwenye masuala yasiyo na tija, tumieni muda wenu kwenye masuala ya shule, msigeuze vyuo kuwa sehemu za siasa, siasa mtazikuta tu, pigeni shule msiingie kwenye mikumbo, kila moja ana maisha yake na baba yake na mama yake, someni, pasua, kazingatieni hilo, nataka niwaeleze kiukweli, kama kutatokea chuo chochote kinafanya fujo, mimi wala sitasita kufukuza, na nikifukuza sifahamu ntawarudisha lini, hili siwatishi nawaeleza ukweli", amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli ameendelea kwa kusema kwamba serikali kupitia wizara ya elimu itahakikisha inkilinda chuo cha Sokoine kama mboni ya jicho, kutokana na upekee ulionacho chuo hiko.

Labels:

Friday, May 4, 2018

Rais JPM Aomba Msaada Serikali ya Denmark




Rais John Magufuli ameiomba Serikali ya Denmark kusaidia ujenzi wa kipande cha barabara ya kilomita 11 katika Mkoa wa Iringa ili kuwezesha malori kutopita katikati ya mji huo ikiwa ni pamoja na kupunguza ajali zinazotokea.

Rais Magufuli ombi hilo wakati akizindua barabara ya Iyovi – Iringa – Mafinga yenye urefu wa kilomita 218 iliyojengwa kwa mkopo nafuu kutoka serikali ya Denmark na kugharimu Sh283 bilioni.

Akitoa maelezo wakati akiomba msaada huo Dk. Magufuli amesema mpango huo ulikuwepo tangu alipokuwa wizara ya ujenzi na kufafanua kwamba malori yanayopita katikati ya mji wa Iringa yamekuwa yakisababisha ajali ndani ya mji wa huo.

“Nakuomba Balozi, hili mlichukue kama la urgent, mkitusaidia kama mkopo sisi tuko tayari, mkitupa kama msaada tutashukuru zaidi. Kwa hiyo tunaomba utufikishie hili, ikiwezekana barabara hiyo tutaiita Pamela Road,” amesema

Mbali na hayo Rais ameweka wazi kwamba "Ujenzi wa barabara hii umegharimu bilioni 283.71 nimekopa kutoka Denmark, mbali na kufadhili mradi huu ilisaidia kukarabati barabara za Chalinze - Mlandizi, Chalinze - Segera, kwa niaba ya watanzania natumia fursa hii kutoa shukrani zangu".

Labels:

Wanaowafukuza Walimu wa Kuu Kisa Matokeo Mabaya ya Shule Kushughulikiwa


Wanaowafukuza Walimu wa Kuu Kisa Matokeo Mabaya ya Shule Kushughulikiwa



Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ufundi, Prof. Joyce Ndalichako, amewajia juu baadhi ya watumishi wa serikali ambao wanatabia ya kuwafukuza kazi walimu wakuu wa shule ambao hutoa matokeo mabaya katika mitihani ya Taifa.

Ndalichako amesema hayo wakati akijibu hoja za wabunge kuhusu bajeti ya wizara yake na kuongeza watumishi hao hasa maofisa elimu, wanajukumu la kusimamia elimu katika eneo husika na sio kuwatupia lawama walimu pindi matokeo yanapokua mabaya.

“Hiyo sio sawa ni uonevu kwa wakuu wa shule kwa sababu na wenyewe wana viongozi juu yao, kwa nini wao ambao wanatakiwa kuwasimamia wasiwajibishwe, ninaagiza maofisa elimu wafanye kazi yao vizuri, utakuta mtu ana shule tano unashindwaje kuzisimamia, kwa hiyo katika hili serikali itahakiksha tunaimarisha usimamizi ikiwa ni pamoja na kuondoa viongozi ambao ni mizigo” amesema Ndalichako

Ndalichako ameongeza kwamba kama serikali inachukua hatua kubwa ili kuimarisha ubora wa elimu lakini baadhi ya watendaji hao wamekua wakirudisha nyuma jitihada hizo na serikali haitasita kuchukua hatua kwa watendaji hao.

Kwa upande mwingine Waziri Ndalichako ameitaka Tume ya Elimu ya Vyuo Vikuu (TCU) pamoja na Baraza la Taifa la Mafunzo ya Ufundi (NACTE) kuhakikisha wanafuatilia ubora elimu ya juu ili kutoa wahitimu wenye sifa zinazostahili na kiwango cha elimu husika.

Labels:

Wednesday, May 2, 2018

Rais JPM Ahoji Jambo Hili " Kwani Kusoma ndo Kujua Kingereza"




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.John Pombe Magufuli amehoji wanafunzi wa chuo cha Mkwawa kwamba kujua kusoma ni kujua Kiingereza.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Mei 2 wakati akizungumza na wanafunzi pamoja na wafanyakazi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, kilichopo mkoani Iringa wakati akitoa ufafanuzi wa shule za private na shule za Sekondari.

“Eti mtu amemaliza form 4 hajui kuandika barua ya kingereza. Kwani kusoma ni kujua kingereza? Wachina wanajua kingereza? mbona wanatengeneza mashine,” amehoji Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amesema kuwa “Shule za private wanafunzi wake wanachujwa, wakifika form 2 kuingia form 3 wanawachuja tena. Wanabaki na ile cream ili waonekane wanaongoza. Serikali inayowapenda wananchi wake haiwezi ikafanya hivyo.”

Labels:

Wednesday, April 25, 2018

Maxcom yatoa Ufafanuzi Utata Tiketi za Mabasi ya Mwendokasi


Maxcom yatoa Ufafanuzi Utata Tiketi za Mabasi ya Mwendokasi...Kumbe UDA-RT Hawajawalipa


Maxcom yatoa Ufafanuzi Utata Tiketi za Mabasi ya Mwendokasi...Kumbe U DART Hawajawalipa

Soma Hapa Chini:






Instal

Labels:

Tuesday, April 24, 2018

ACT Wazalendo Wafunguka ishu ya 'Kufichwa Zitto Kabwe'


ACT Wazalendo Wafunguka ishu ya 'Kufichwa Zitto Kabwe' Baada ya Kuikosoa Ripoti ya CAG




ACT Wazalendo kupita kwa Katibu wa Uenezi wa Chama hicho Ado Shaibu kimefunguka na kuweka wazi kuwa Kiongozi Mkuu wa chama hicho Mhe. Zitto Kabwe hajafichwa kama ambavyo watu wanasema bali sasa hivi ameongezewa ulinzi na mienendo yake inaangaliwa kwa kina na idara ya ulinzi na usalama.

Ado Shaibu amedai kuwa zipo taarifa zinaenea kwenye mitandao ya kijamii mbalimbali kuwa kiongozi huyo anaweza kuuawa na kusema ndiyo sababu kubwa ambayo imepelekea sasa kulindwa kwa daraja la juu kabisaa la ulinzi.


"Ukisikia kwamba kiongozi wenu anataka kushambuliwa, kudhuriwa au kuuwawa ni muhimu kuyapa uzito sana maneno hayo kwa hiyo sisi tumechukua hatua kadhaa kwanza ndugu Zitto alikuwa na mkutano wa hadhara Kigoma Ujiji alikuwa anataka kuzungumzia masuala yanayoendelea nchini kuhusu ripoti ya CAG lakini alitaka kuwaeleza watu wa Kigoma wapi amefikia kuhusu suala la watu wa Kigoma kunyanyaswa uhamiaji na kutaka maoni ya wananchi kwa hiyo mkutano wenyewe huo ulizuiwa na sisi tulikuwa na mkutano wa ndani wa chama kutokana na mambo haya yanayoendelea tukaamua ni bora tusimamishe kikao hicho" alisema Shaibu
Ado Shaibu aliendelea kusema kuwa


"La pili kiongozi wa chama ameongezewa ulinzi na idara ya ulinzi na usalama ya chama kuhakikisha kwamba anakuwa salama na kuchunga mienendo yake ndiyo maana utaona baadhi ya magazeti yanasema Zitto Kabwe amefichwa, ndugu Zitto ni kiongozi hawezi kufichwa lakini mienendo yake sasa inadhibitiwa na idara ya ulinzi na usalama ya chama awe wapi, muda gani na kwanini, awe ndani ya nchi, nje ya nchi hayo ndiyo mambo ambayo idara yetu ya ulinzi na usalama inayapa kipaumbele kikubwa, kwa hiyo kiongozi sasa analindwa kwa daraja ya juu" alisisitiza Ado Shaibu
Baada ya Zitto Kabwe kuonekena ameikomalia sana ripoti ya CAG hasa zaidi kuhusu 1.5 Trilioni ambayo haileweki imetumikaje zilianza kusambaa taarifa mbalimbali kuwa kiongozi huyo naye anaweza kushughulikiwa na watu wasiojulikana.

Labels:

Monday, April 23, 2018

Rais Magufuli afanya uteuzi wa benki


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Edmund Bernard Mndolwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Posta Tanzania (TPB).


Uteuzi wa Dkt. Mndolwa umeanza leo tarehe 23 Aprili, 2018.


Labels:

Friday, April 20, 2018

Mfalme wa Swaziland abadili jina la nchi hiyo




Mfalme Mswati wa III wa Swaziland amebadilisha jina rasmi la taifa hilo kutoka Swaziland na kuliita Ufalme wa eSwatini (The Kingdom of Swaziland) wakati wa maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa ambapo ametimiza miaka 50 na wakati huo huo taifa hilo likiadhimisha miaka 50 ya uhuru wake.

Jina hilo jipya, eSwatini, lina maana ya ardhi ya Waswaz na limetumiwa rasmi na Mfalme Mswati wa III kwa miaka mingi. eSwatini ni jina ambalo mfalme alilitumia alipokuwa akihutubia katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 2017 na katika ufunguzi wa bunge la nchini mwake mwaka 2014.

Mfalme Mswati ni miongoni mwa wafalme wa mwisho wa duniani waliobaki na ametawala tangu mwaka 1986.

Mswati III kwa sasa ana wake 15 akiwa anaifuata rekodi ya Baba yake aliyekuwa na wake 125. Wanaharakati wa kutetea usawa wa jinsia wanasema mfumo wa utawala wa nchi hiyo ni wa kushangaza na unawabagua wanawake.

Mswati III ametoa sababu kuu ya kubadilishwa kwa jina la nchi yake kuwa kila aendapo katika mikutano ya kimataifa, mataifa mengine wamekuwa wakilichanganya taifa lake na nchi ya Switzerland.

Nao raia wametoa maoni yao juu ya hatua ya mfalme wao na kusema kuwa badala ya kushughulika na jina la nchi yake, badala yake alipaswa kupasua kichwa ni namna gani anaweza kuimarisha uchumi wa nchi hiyo unaodidimia siku hadi siku.

Kwa taarifa yako, Mfalme Mswati anajulikana pia kama Ngwenyama kwa lugha ya taifa hilo jina likiwa na maana ya ‘Simba’, lakini pia anajulikana ulimwenguni kwa tabia yake ya kuoa wake wengi na kwa kuzingatia mavazi ya jadi pamoja na kuthamini mila na desturi.

Labels:

Zitto: Serikali Inasema Uongo

Zitto: Serikali Inasema Uongo, Ni Muhimu Bunge Lichunguze Ziliko 1.5 Trilioni


Taarifa Ndogo ya ACT Wazalendo Juu ya Majibu ya Serikali Bungeni Juu ya Ziliko 1.5 Trilioni Zisizoonekana Matumizi yake Kwenye Ripoti ya CAG

Tumesoma majibu ya Serikali kuhusu hoja ya Ukaguzi wa shilingi 1.5 trilioni za umma ambazo hazijulikani zilipo kama yalivyosomwa na Naibu Waziri wa Fedha asubuhi hii bungeni. Ni maelezo yale yale aliyoyatoa Katibu Mwenezi Taifa wa CCM, ambayo tayari jana yamejibiwa na Katibu Mwenezi Taifa wa ACT Wazalendo, ndugu Ado Shaibu.

Kwa sasa tuna machache tu ya kueleza:

1.Serikali imesema uongo. Taarifa ya Serikali ya leo na Taarifa ya Fedha ya Benki Kuu, wanaotunza Fedha za Serikali hazisomani kabisa. Tutaongea na waandishi kueleza hili kwa undani zaidi. Ijulikane tu kuwa akaunti za Serikali kwenye Taarifa za Fedha za Benki Kuu hazina hizo Fedha Naibu Waziri ametaja.

2.Ni dhahiri kuwa kuwa ubadhirifu mkubwa wa Fedha za Umma, ndio maana taharuki ya Serikali ni kubwa, kiasi cha majibu ya Serikali kupewa Kiongozi wa CCM kuyasema, na kwa kuwa kashindwa kukonga nyoyo, sasa imebidi Serikali ije yenyewe kuyasema majibu yale yale yaliyosemwa na CCM. 

Tunashuhudia Kwa mara ya kwanza Zanzibar ikikusanyiwa zaidi ya TZS bilioni 200 Sawa na 20% ya Bajeti nzima ya Zanzibar, makusanyo yote ya TRA Zanzibar na mara 10 ya makusanyo ya Zanzibar kutoka PAYE za Muungano ambazo ndio pekee hukusanywa na TRA. Uongo huu wa Serikali ya CCM lazima unasukumwa na Wizi. Zanzibar hukusanyiwa TZS bilioni 21 tu na TRA, 200B zatoka wapi? Balaa

3.Sisi ACT Wazalendo, tunaendelea kumsihi Spika wa Bunge aruhusu Ukaguzi Maalum wa matumizi ya Shilingi 1.5 trilioni kupitia Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, PAC, kwani hata haya majibu ya Serikali yanapaswa kuhakikiwa kwanza na CAG kabla ya kusomwa Bungeni, jambo ambalo halikufanyika. PAC wanajua kuwa makusanyo ya Serikali ni CASH BASIS na sio accrual. Serikali imedanganya, lazima PAC sasa wafanye kazi yao.

Muhimu: Tamko la Serikali ni matusi Kwa CAG. Watanzania mjiandae kuilinda Taasisi ya Ukaguzi wa Taifa. Serikali ya CCM inataka kuivunja vunja taasisi hii ya uwajibikaji. Tusikubali.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Aprili 20/2018


Labels: