Tuesday, March 20, 2018

Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwaka 1922 , katika kijiji cha Butiama, wilaya ya Musoma, mkoa wa Mara. Alikuwa moja kati ya watoto 26 wa Nyerere Burito, chifu wa kabila la Wazanaki. Alipokuwa mtoto Nyerere alichunga mifugo ya babake; katika umri wa miaka 12, aliingia shule akitembea kilomita 30 hadi katika shule ya msingi ya Mwisenge, iliyoko Musoma Mjini.



Baada ya kumaliza masomo ya ualimu alirudi Tabora akifundisha shule ya sekondari ya Mtakatifu Maria (St.Mary´s), Mwaka 1949 alipata skolashipu ya kwenda kusoma kwenye Chuo Kikuu cha Edinburgh huko Uskoti / Uingereza akasoma Shahada ya Uzamili ya historia na uchumi, kwa hatua hiyo Mwalimu alikuwa mtanzania wa kwanza kusoma katika chuo kikuu cha Uingereza na mtanzania wa pili kupata shahada ya elimu ya juu nje ya Tanzania.

kutokana na ujasiri na nia ya kuwa mwelewa wa kila kitu ya Nyerere, Mapadre wa Kanisa katoliki wakaona akili yake na nia yake nzuri ya kutaika kujifunza wakamsaidia kusoma kozi ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere, Kampala, Uganda kuanzia mwaka 1943 hadi 1945.akiwa katika Chuo cha Makerere akaanzisha tawi la Umoja wa wanafunzi Watanganyika pia akaamua kujihusisha na tawi la Tanganyika African Association (TAA).

Baada ya kumaliza shule ya msingi aliendelea kusoma shule ya wamisionari Wakatoliki iliyoko Tabora. Katika umri wa miaka 20, Nyerere alibatizwa akawa mkristo Mkatoliki hadi mwisho wa maisha yake.

Aliporejea Tanganyika kutoka masomoni, Nyerere alifundisha Historia, Kingereza na Kiswahili katika shule ya St. Francis iliyo karibu na Dar es Salaam, (siku hizi Pugu Sekondari). Mwaka 1953 alichaguliwa kuwa rais wa chama cha Tanganyika African Association (TAA), chama ambacho alikisaidia kukijenga alipokuwa mwanafunzi katika huo kikuu cha Makerere. Mwaka 1954, alikibadilisha chama cha TAA kwenda katika chama cha Tanganyika African National Union (TANU) ambacho kilikuwa cha kisiasa zaidi kuliko TAA. Ndani ya mwaka mmoja chama cha TANU kilikuwa tayari chama cha siasa kinachoongoza Tanganyika.

Uwezo wa mwalimu uliwashitua viongozi wa kikoloni na kumlazimisha Nyerere kuchagua kati ya siasa na kazi ya ualimu. Nyerere alisikika akisema kuwa alikuwa mwalimu kwa kuchagua na mwanasiasa kwa bahati mbaya. aliamua kujiuzulu ualimu na kuzunguka nchini Tanganyika kuzungumza na watu wa kawaida na machifu ili kuleta muungano katika mapigano ya uhuru.

Pia alizungumza kwa niaba ya TANU katika Mkutano wa Baraza la udhamini (Trusteeship council) ya Umoja wa Mataifa (UN) huko New York. Uwezo wake wa kimaongezi na kuunganisha watu ulimwezesha kufanikisha Tanganyika kupata uhuru bila umwagaji wa damu. Ushirikiano mzuri aliouonyesha aliyekuwa gavana wa wakati huo Richard Turnbull, ulisaidia pia kuharakisha upatikanaji wa uhuru.

Nyerere aliingia katika bunge la kikoloni mwaka 1958 na kuchaguliwa kuwa waziri mkuu mwaka 1960. Mwaka 1961 Tanganyika ilipata uhuru wake na Desemba 9,1961 Nyerere alichaguliwa kuwa waziri mkuu wa Tanganyika huru na mwaka mmoja baadae Nyerere alikuwa raisi wa kwanza wa jamhuri ya Tanganyika. Nyerere alikuwa kiungo muhimu katika katika muungano wa Tanganyika na Zanzibar kutengeneza Tanzania baada ya mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964, yaliyomtoa madarakani sultani wa Zanzibar Jamshid bin Abdullah.

Hayati Mwalimu Nyerere mnamo Februari 5, 1977, aliongoza chama cha TANU katika tendo la kuungana na chama tawala cha Zanzibar ASP na kuanzisha chama kipya cha CCM (Chama cha Mapinduzi) akiwa mwenyekiti wake.

Nyerere aliendelea kuongoza Taifa hadi 1985 alipong,atuka na kumwachia nafasi rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi.

Aliendelea kuongoza Chama cha CCM hadi 1990 na kuwa na makini na mfuatiliaji huku akionya katika mambo kadhaa katika siasa ya Tanzania hadi kifo chake.

baada ya kustaafu kazi ya ukuu wan chi, Nyerere alikaa muda mwingi kijijini kwake alikozaliwa Butiama akilima shamba lake la mahindi. Pamoja na haya alianzisha taasisi yenye jina lake inayojulikana kama “Mwalimu Nyerere Foundation, mwaka 1996 alionekana akiwa mpatanishi wa pande mbalimbali wa vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Burundi.

Mwishoni mwa maisha yake Mwalimu aliishi kama mkulima wa kawaida kijijini kwake Butiama

Mwalimu alianza kujisikia vibaya mwezi Augost mwaka 1999, akaanza kupata matibabu ya kila mara baadaya alihamishiwa katika Hospitali ya Mtakatifu Thomas huko Uingereza.

Oktoba 14, 1999 aliaga dunia katika hospitali hiyo ambapo madaktari walisema kuwa alikuwa akisumbuliwa na kansa ya damu ( leukemia).


Mafanikio na kasoro

Kitendo kikubwa ambac ho hakisahahuliki ambacho Mwalimu alikifanya na dunia inakumbuka ni kuchanganya ardhi za Zanzibar na Tanganyika ambapo Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ulizaliwa rasmi na hadi leo upo.

Kujenga umoja wa kitaifa na utamaduni wa Kiafrika pamoja na lugha ya Kiswahili, kushinda ubaguzi wa rangi, kutetea usalama wa taifa katika vitani dhidi Nduli Idi Amin Dada wa Uganda.

watu walimuita mwalimu kuwa ni mwanamapinduzi wa afrika, kiongoiz wa bara nzima kutokana na nia zake za kutaka kila Mwafrika kuwa huru na kuwa na amani.

Mwalimu pia alifanikiwa kutoa mchango kwa vyama vya ukombozi vya nchi za kusini ya Afrika kama; Zimbabwe {ZANU), Afrika Kusini (ANC na PAC), Namibia (SWAPO), Angola (MPLA) na Msumbiji (Frelimo)

Kutofanikiwa kwake

Kitu ambacho kilimuumiza mwalimu na kumfanya akose raha mara nyingi ni juu ya kutofanikiwa kwa nia yake ysa kuanzisha siasa za Kijamaa. Siasa zake za ujamaa zilishindwa baada ya mwaka 1976.

Baada ya kuona kuwa uchumi wa Tanzania hautaweza kusimama kwa siasa za kijamaa na kutoweza kuvumilia kuendesha nchi kwa siasa ambazo yeye hakuwa muumini, Nyerere kwa maamuzi yake mwenyewe aliamua kustaafu nafasi ya urais baada ya uchaguzi wa mwaka 1985 na kumwachia usukani kwa Mwinyi aliyetawala kwa siasa za uchumi wa soko huria.

Katika hali ya kukubali ukweli, Nyerere alitamka katika tafrija ya kumwaga juu ya siasa yake kiuchumi “Nimefeli. Tukubali hivyo.”

Alikosolewa pia
Kutokana na hali hiyo na kufikia yeye kukubali kushindwa Mwalimu Nyerere analaumiwa kwa siasa zake za kiujamaa kuwa zilichelewesha maendeleo ya kiuchumi wa Tanzania, Pamoja na kwamba hata leo kuna makundi ya watanzania kwa mtazamo wao yanazitamani siasa hizo.

Pia kuna makundi ya waislamu wanaomtuhumu kwa kuendesha kwa siri vita dhidi ya uislamu na upendeleo wa elimu na madaraka kwa wakristo.

Kutangazwa mwenye Heri

Kwa taratibu za Kanisa Katoliki, mchakato wa kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa mtakatifu ulianza mwaka 2005, na tayari kanisa hilo kwa kibali rasmi kutoka Roma makao ya Baba Mtakatifu, limeshamtangaza kuwa mwenyeheri.


Kuwa mwenyeheri ni hatua ya kwanza ya kuingia utakatifu. Wakristo wakatoliki wameanzisha sala maalumu na kufanya maombi kwa nia ya maombezi yake ili aweze kutangazwa kuwa mtakatifu.


Ibada ya kwanza ilifanyika katika kanisa kuu la Jimbo la Musoma, na kuongozwa na aliyekuwa askofu wa Jimbo hilo marehemu askofu Justine Samba.

Alikuwa mwanamichezo

Licha ya Kuwa mwalimu na mwanasiasa hususani kiongozi mkuu wan chi, pia Nyerere alikuwa mwanamichezo, aliazznisha mchezo wa Bao, akiwa Butiama alicheza bao nyumbgani kwake na majirani zake, wakati mwingine alipotembelewa na wafuasi wake wa kisiasa alikuwa akishiriki nao kucheza bao.

Kutokana na maisha yake aliyoyaishi ambayo yalijaa uvumilivu, unyenyekevu na uadilifu bado anakumbukwa na watanzania hasa wa hali ya chini hasa kutokana na sera zake za kujali utu na ubinadamu.

Ni mmoja wa viongozi wachache wanaokumbukwa kwa kutojilimbikizia mali pamoja na kutawala kwa miaka zaidi ya 24.

Source: Articles on Julius K. Nyerere

Labels:

Rolihlahla Mandela


Mandela alisoma katika Chuo Kikuu cha Fort Hare na Chuo Kikuu cha Witwatersrand. Akawa mwanasheria mwaka 1942. Mwaka 1944, alijiunga na Chama cha ANC, chama kilichodhamiria kuutokomeza utawala wa makaburu weupe pekee. Mwaka 1960, Chama tawala cha makaburu kilikipiga marufuku cha cha ANC na kuwashitaki viongozi wake kwa kosa la uhaini, lakini Mandela aliachiwa huru.


MAJINA YA UTANI: Madiba, Black Pimpernel
MAHALI ALIKOZALIWA: Mveso, Transkei, South Africa
KAZI: Mwanaharakati, Kiongozi wa dunia
TAREHE YA KUZALIWA: Julai 18, 1918
TAREHE YA KUFA: DESEMBA 05, 2013
MAHALI ALIKOFIA: Johannesburg, South Africa
ELIMU: Taasisi ya Clarkebury, Chuo cha Wesleyan, Chuo Kikuu Kishiriki cha Fort Hare, Chuo Kikuu cha London, Chuo Kikuu cha Witwatersrand, Johannesburg.

Rolihlahla Mandela

KUFUNGWA GEREZANI
Akiendeleza harakati zake za kupambana na makaburu, Mandela alikamatwa, akatiwa hatiani na kuhukumiwa kifungo cha maisha gerezani kuanzia mwaka 1964 hadi 1990, ambapo maisha yake kama kiongozi wa harakati za kupambana na ubaguzi wa rangi yakajulikana dunia nzima. Kama mfungwa wa dhamiri, Mandela mara kwa mara alikataa kuachiwa kwa masharti.

KUACHIWA HURU
Mwaka 1990, akiwa amekaa jela kwa miaka 26 na akiwa na umri wa miaka 71, iliachiwa huru bila masharti yoyote baada ya utawala wa kibaguzi kushinikizwa na jumuiya ya kimataifa. Mwaka 1993, Nelson Mandela alishinda Tuzo ya Nobel kwa harakati zake za kisiasa.
The late Rolihlahla Mandela with his family members

Labels:

Sunday, March 18, 2018

Che Guevara






HISTORIA FUPI YA CHE GUEVARA

Jina kamili : Ernesto Guevara
Kazi : Daktari, mwanamapinduzi wa kijamaa (marxist)
Uraia : Argentina
Kuzaliwa : June 14 1928
Kufariki : October 9, 1967 ,Bolivia milima ya La heguera
Chanzo cha kifo : kuuwawa kwa kupigwa risasi


Kama kijana msomi wa shahada ya udaktari, che Guevara alisafiri nchi nyingi sana huko bara la Amerika ya kusini na rafiki yake, akawa ni mtu mwenye uchungu mkubwa kuona maisha ya dhiki,njaa, magonjwa nchi za America ya kusini, akawa na mwamko mkubwa kubadili hali ile kwa kuwa aliamini ya kuwa mfumo wa ubepari ndio chanzo kikubwa kilichokuwa kinaitafuna Latin America.

Miaka ya 50 akiwa anasoma udaktari huko Mexico Che Guevara alikutana na Fidel Castro na Raul Castro ambapo watatu hao walipanga mapinduzi ya kumg’oa raisi wa Cuba wakati huo Fulgencio batista ambaye alikuwa na huhusiano wa kimaslahi na America, Che akapata nguvu na uaminifu mkubwa kutoka kwa Fedel Castro na kupandishwa kuwa kiongozi wa wanamgambo (guerilla insurgents)

Punde tu baada ya Fulgencio batista kukimbia CUBA,Che alihusika kama mtu muhimu katika serikali ya Cuba iliyoongozwa na Fidel Castro, akiwa kama Gavana wa benki kuu ya Cuba ambapo saini yake ilianza kutumika katika noti za CUBA , baadae kama waziri wa kilimo wa Cuba.

Mwaka 1964 akiwa kama mmoja ya msafara wa watu wa serikali ya Cuba umoja wa Mataifa New York MArekani, aliweza kupata “sifa” ya “mwanamapinduzi halisi wa kukumbukwa” pale alipotoa hotuba ndefu katika ukumbi wa UN akilaumu wazi ukimya wa Umoja huo juu ya kilichokuwa kinaendelea Afrika ya kusini (ubaguzi wa Rangi) alinukuliwa akisema

“wale wanaoua watoto wao na kuwabagua kila siku kwa sababu ya rangi ya ngozi zao, wazungu wanawaua watu weusi na hawakamatwi, serikali ya kikaburu inawalinda wauaji, na mbaya Zaidi inawaadhibu watu weusi kwa kuwa tu wanatataka haki zao na utu wao, vipi watu hawa (makaburu) wakaitwa watetezi na walinzi wa Amani?”

MGOGORO WA CONGO – DRC

miezi michache baada ya kutoa hotuba UN, Che alitoweka katika maisha ya kawaida “public life” na hakuna aliyejua alikwenda wapi mpaka baadae ilipokuja gundulika Che alikuwa akipigana sambamba na Laurent Kabila huko Congo dhidi ya wabeligiji na baadhi ya wapiganaji wa ki cuba waliokuwa Afrika, vita ambayo ilishindikana na akakimbilia Tanzania na kukaa maeneo ya karibu na ziwa Tanganyika na baadae Dar es salaam huku akiishi kwa kujificha

baadae mwaka 1966 alirejea Cuba kumuaga Fidel castro na kusafiri kwenda Bolivia kuendeleza harakati zake za kuzikomboa nchi za America ya kusini kutoka kwenye makucha ya Ubepari…aliingia Bolivia akiwa kama mfanyabiashara asiyejulikana baada ya kunyoa upara, kuweka mvi bandia na kuyoa ndevu zake zote, akaweka kambi na baadhi ya wapiganaji wenzake aliowakuta Bolivia maeneo ya milima ya montane dry fores

KUKAMTWA NA KUUAWA

Mwaka 1967, makachero wa Bolivia wakisaidiwa na CIA ambaye alikuwa akiwakilisha ndugu Felix Rodriguez waligundua maficho yake na kundi lake huko milimani Bolivia, asubuhi ya October 8 mwaka 1967 wanajeshi takribani 1,800 walizingira maeneo yoote ya milima walikokuwa wamejificha akina Che Guevara na ikapiganwa vita ya masaa kadhaa na Che Guevara akipigwa Risasi za miguu na kukamatwa na wenzake.

Yasemekana baada ya kuzidiwa katika mapigano yale alisema
“Usifyatue risasi, mi ni Che Guevara nina thamani kubwa kuwa hai kuliko kunikamata nimekufa”

Alifungwa kamba na wenzake akakamatwa na kupelekwa kijiji cha La higuera ambapo baada ya raisi wa Bolivia ndugu kusikia amekamtwa alitoa amri auwawe haraka sana, wakati huo huo CIA walimtaka apelekwe Panama akahojiwe kwa kina na salama yake ili hasiuwawe alikuwa apelekwe America japo haikutokea.
Siku moja kabal ya kuuwawa alichukuliwa na baadhi ya wanajeshi na kupiga picha ya kumbukumbu na kesho yake akauliwa na askari mmoja aliyejitolea na kumpiga risasi sita za kifua na kufa palepale

Kabla hajapigwa risasi na muuaji wake haya ndio yalikuwa maneno yake ya mwisho
“Najua umekuja kuniua, shoot mtu mwoga wewe!!! na ufahamu utakua umeua mwanaume kamili”

Aliacha wake wawili na watoto watano

Labels:

Thursday, March 8, 2018

N! XAU-TOMA (Bush Man)


Mfahamu N! XAU-TOMA (Bush Man) Mhusika mkuu wa Filamu ya ”The Gods Must Be Crazy”

N! XAU ǂTOMA, Alizaliwa Desemba 16, 1944, alikuwa Mnamibia na muigizaji ambaye alikuwa akiishi porini, alikuwa maarufu baada ya uhusika wake kama Mhusika Mkuu katika filamu ya THE GODS MUST BE CRAZY, Iliyoigizwa mnamo mwaka 1980 ambapo yeye alicheza kama mtu kutoka Jangwa la Kalahari, na watu wa Namibia walimfahamu yeye kama Muigizaji Maarufu kuliko wote Nchini Namibia.



N!xau alikuwa mwanachama wa SAN (Wenyeji wa Maeneo ya Jangwa la Kalahari), ambao pia walijulikana kama BUSH MEN.

Alikua na uwezo wa kuongea kwa ufasaha Lugha au Makabila takribani matatu yanayopatikana maeneo ya Namibia yaani ki-Ju|’hoan, Ki- Otjiherero na Ki-Tswana.

Kutokana na Mwenendo wa Maisha ya porini aliyoishi, yeye mwenyewe hakujua umri wake halisi, na kabla ya kuonekana katika filamu ya THE GODS MUST BE CRAZY, Bush man alikuwa na uzoefu kidogo sana wa maisha ya kisasa, alikuwa amewahi kuwaona watu weupe (Wazungu) watatu tu, na alikuwa hajui thamani ya fedha ya noti , (kwa mujibu watovuti ya Legend) fedha ambazo angepata katika mapato yake ya kwanza katika Filamu ya THE GODS MUST BE CRAZY alikuwa tayari kuziacha zikaenda na upepo maana hakujua matumizi yake.

Katika filamu hiyo ya kwanza mwaka 1980 alipata kiasi cha Dola 300 za Kimarekani, muda huo alifundishwa thamani ya fedha katika Ulimwengu na hivyo Filamu zilizofuata aliweza kufanya makubaliano ya kuigiza na kupata malipo makubwa kufikia Rand za Afrika kusini R800,000. Japo hakuwa na uelewa wa matumizi ya pesa bado aliweza kujenga nyumba nzuri kwa ajili ya familia yake.

Baada ya kuachana na mikataba ya kazi yake ya filamu katika mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo China na Marekani, alirudi Namibia, ambako alilima mahindi, maboga na maharage na kufuga ng’ombe kadhaa (lakini si zaidi ya 20 wakati huo, kwa sababu kwa mujibu wa Tovuti ya Independent, bila mifumo ya kisasa ya kilimo yeye alikuwa anapata shida sana katika ufugaji wa ng’ombe zaidi ya hao zaidi), ila baadae jarida la Namibia liitwalo NEW ERA lilisema kuwa hakuwa na uwezo wa kuhesabu zaidi ya 20.

Katika hatua nyingine, mwezi Julai mwaka 2000 N! XAU Aliingia rasmi katika dini ya Kikristo, na baadae alibatizwa na kuwa Mu-Adventista Msabato.





Tarehe 5 Julai 2003, alifariki kutokana na magonjwa sugu ya kifua yaliyoambatana na kifua kikuu, wakati hou alikuwa akijihusisha na uwindaji wa ndege aina ya Kanga.

Kulingana na makadirio rasmi alikuwa na umri wa miaka kati ya 58 au 59 wakati huo, na alizikwa Julai 12 huko Tsumkwe karibu na kaburi la mke wake wa pili. Na alikuwa na watoto sita waliokuwa hai.

FILAMU ALIZOIGIZA
The Gods Must Be Crazy (1980) (Actor)
The Gods Must Be Crazy II (1988) (Actor)
Kwacca Strikes Back (1990) (Actor)
Crazy Safari (1991) (Actor)
Crazy Hong Kong (1993) (Actor)
The Gods Must be Funny in China (1994) (Actor)
Sekai Ururun Taizaiki (1996) (Himself)

Reference CLICK HERE

Labels: