Friday, May 11, 2018

Serikali Yafunguka Sakata la Ugonjwa wa Ebola




Serikali imesema hakuna mgonjwa yeyote aliyehisiwa au kuthibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa wa Ebola hapa nchini na kuwataka wananchi kuchukua tahadhari kubwa dhidi ya ugonjwa huo ambao umeripotiwa hivi karibuni katika nchi jirani ya Demokarasia ya Kongo (DRC).


Kauli hiyo imetolewa leo na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

Waziri Ummy amesema kuwa hata hivyo taarifa hiyo haizuii Tanzania kuchukua hatua thabiti dhidi ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola kwa kuwa inapakana na nchi ya DRC ambapo kuna mipaka mingi ambayo watu huwa wanaingia na kutoka kwa njia zisizo za halali.

"Tanzania imepokea taarifa ya uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini DRC uliotangazwa na na shirika afya Duniani Mei 8 mwaka huu ambapo vipimo vya maabara vimethibitisha baada ya kupokea wagonjwa 21 ambapo kati yao 17 wamepoteza maisha", amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewataka watu wanaoishi katika mikoa inayopakana na nchi ya DRC kuchukua tahadhari pale wanapohisi kupata magonjwa yenye dalili za Ebola kwa kuwahi kufika kwenye hospitali zinazotoa huduma ili wafanyiwe vipimo vya kina kuonyesha kama wameathirika au la.

Waziri Ummy ameitaja mikoa ambayo inapakana na nchi ya DRC kuwa ni Mwanza, Kagera, Kigoma, Katavi, Rukwa na Songwe na kuwataka wananchi wanaoishi katika mikoa hiyo kuchukua tahadhari kubwa ya kujikinga na ugonjwa wa Ebola.

“Nimeitaja mikoa hiyo kwa sababu ina njia nyingi ambazo siyo rasmi zinazowawezesha watu kuvuka kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine na hivyo kama kutakuwa na mtu ambaye ameambikizwa ugonjwa huo itakuwa ni rahisi kuusambaza tofauti na mtu nayeingia nchini kwa kutumia mipaka rasmi kama vile uwanja wa ndege”, amesema Waziri Ummy.

Kwa upande mwingine, Waziri Ummy amesema Wizara imechukua hatua mbalimbali ili kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo kutoa taarifa ya tahadhari ya ugonjwa wa Ebola kupitia kwa makatibu tawala na waganga wakuu wote wa mikoa kwa kujumuisha na namna mgonjwa anavyoweza kutambuliwa, namna ya kuchukua sampuli na namna ya kuwahudumia wagonjwa.

Labels:

Wednesday, April 25, 2018

Waziri wa Afya Apiga Marufuku Kuuza Dawa za Maralia




Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeendelea na msisitizo wa vituo vya Afya, Zahanati na Hospitali za serikali kuacha tabia ya kuuza dawa za kutibu malaria nchini na endapo mtoa huduma ataenda kinyume na hilo atachukuliwa hatua stahiki dhidi yake.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu wakati alipotembelea Zahanati ya Mwandiga iliyopo wilayani Kigoma Mkoa wa Kigoma katika akiwa anangalia hali ya matibabu dhidi ya malaria wilayani humo kuelekea kilele cha siku ya Malaria Duniani.

"Nawaagiza waganga wakuu wa Mikoa na Wilaya kuweka matangazo yanayooonyesha kipimo cha haraka cha Malaria, dawa za kutibu Malaria ya mseto na sindano ya kutibu malaria kali ni bure kwenye kila zahanati, kituo cha afya na hospitali ya serikali", amesema Waziri Ummy.

Aidha, Waziri Ummy amewataka waganga wakuu wa vituo ngazi za zahanati na waganga wakuu wa wilaya waweke namba zao za simu kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini ili kuwasaidia Watanzania kutoa malalamiko yao pindi wanapopatiwa huduma ambazo za hazikidhi viwango ili kubendelea kuboresha huduma za afya nchini.

Waziri Ummy amesema kuwa katika kujikinga na Malaria wananchi wanatakiwa kutumia vyandarua vyenye dawa, kusafisha mazingira na kuondoa mazalia ya mbu waenezao ugonjwa huo kwani kinga ni bora kuliko tiba.

Sambamba na hilo Waziri Ummy ametoa vyandarua vyenye dawa ya kukinga dhidi ya Malaria katika kijiji cha Mwandiga ili kuendelea na juhudi za kutokomeza Malaria nchini katika kuelekea siku ya Malaria Duniani.

Labels:

Thursday, April 19, 2018

Majani ya Mstafeli ni dawa bora ya saratani ya tezi dume




Majani ya Mstafeli ni dawa bora ya saratani ya tezi dume

Majani ya mti wa mstafeli yamekuwa yakitumika na watu kwenye misitu ya amazon kwa maelfu ya miaka iliyopita kutibu karibu kila ugonjwa. Ndiyo hii inaweza kuwa ni habari mpya kwako hasa kama wewe siyo mfuatiliaji wa mambo haya ya tiba asili kwa ujumla lakini sasa habari unayo.

Mti huu wa mstaferi ndiyo tiba asili pekee inazungumziwa sana na watu wote duniani kwa sasa kuhusu maajabu yake ya kutibu saratani mbalimbali ikiwemo saratani ya tezi dume.

Na hiyo yote ni kwa sababu nzuri tu ….

Majani ya mti wa mstafeli yanaziua seli za saratani mara 10000 zaidi ya mionzi. Na jambo la ajabu zaidi ni kuwa dawa hii haizidhuru seli hata kidogo tofauti na tiba ya mionzi ambayo inaziua mpaka seli nyingine zenye afya wakati wa matibabu yake.

Yaani dawa hii ya majani ya mstafeli huziwinda seli za kansa na kuziua huku ikikuachia seli zako zenye afya bora zaidi. Kama haitoshi majani ya mstafeli yanaongeza pia idadi na uwingi wa seli zako nyeupe za damu na kuongeza kinga ya mwili kwa haraka sana.

Majani haya yamethibitika siyo kutibu saratani au kansa ya tezi dume bali na aina nyingine za saratani zaidi ya 12 ambazo ni pamoja na:

1. Saratani ya damu
2. Saratani ya matiti
3. Saratani ya mlango wa kizazi
4. Saratani ya mapafu
5. Saratani ya ini
6. Saratani ya mdomo
7. Saratani ya kwenye ulimi
8. Saratani ya kongosho
9. Saratani ya kwenye mji wa uzazi
10. Na sratani nyingine nyingi

Majani ya mstafeli ni dawa nzuri dhidi ya bakteria na fangasi mbalimbali mwilini na hivyo ni kinga dhidi ya maambukizi ya kila namna.

Majani ya mstafeli yanatibu pia:

1. Kisukari
2. Gout (maumivu ya jongo)
3. Maumivu ya mgongo
4. Yanaongeza kinga ya mwili
5. Yanaimarisha afya ya tumbo kwa ujumla
6. Kufunga choo
7. Msongo wa mawazo (stress)
8. Yanaimarisha afya ya nywele
9. Yanaimarisha afya kwenye mfumo wa upumuwaji
10. Yanaongeza afya ya ngozi
11. Mazuri kwa afya ya moyo
12. Yanadhibiti homa na kutuliza joto la mwili

Dawa kubwa ya saratani ambayo watu wengi hawaifahamu …

Kuna wakati namtafakari Mungu na nashindwa kupata majibu kwamba kuna wakati watu wanateseka sana lakini bila sababu yoyote maalumu zaidi ya kukosa tu maarifa.

Kile nitakushangaza kidogo hapa ni kuwa uwezo huu wa majani ya mstafeli kutibu kansa uligundulika tangu mwaka 1976 na taasisi ya saratani ya Marekani lakini matokeo yake hayajawahi kuwekwa hadharani kwa watu!

Kwanini hawakutaka kutangaza kwa watu?

Hakuna mtu anayejuwa kwa hakika sababu ni nini iliyowafanya wabaki na matokeo hayo bila kutangaza kwa watu. Hata hivyo wengi wanaamini ni kutokana na vipimo na matibabu ya ugonjwa huu kuwa ni dili kubwa kwa viwanda vya madawa na biashara kubwa kote duniani.

Sababu kuweza kutibu ugonjwa mkubwa hivyo (kwa mjibu wa maoni yao) kwa kutumia mmea rahisi hivyo kupatikana ni jambo lisilo na faida. Matatizo mengi ya binadamu chanzo chake kikuu cha matatizo hayo ni hela.

Pamoja na hayo Mungu yupo na hatatuacha watu wote tuangamie kijinga hivyo. Wachache atatuokoa tu kwa namna yoyote. Hivyo watu wengi tayari wameanza kugeuka upande huu wa pili na tayari wanaona faida zake.

Utatumiaje majani ya mstafeli kama dawa?

Namna nzuri zaidi na ili kujihakikishia unapata faida zake kwa kiwango cha juu kabisa ni kutumia juisi freshi ya majani haya. Unachohitaji ni kuwa na blenda ya umeme, maji na majani mabichi ya mstafeli. Tengeneza juisi yako tuseme majani 6 unaweza kutengeneza juisi vikombe viwili (nusu lita) na unywe kikombe kimoja (robo lita) kutwa mara kila nusu saa kabla ya chakula cha asubuhi na cha jioni kwa mwezi mmoja mpaka miwili.

Ni dawa nzuri kwa kansa karibu zote pia inaondoa uvimbe wa aina yoyote.

Unaweza pia kutengeneza chai ukitumia majani haya, unaweza pia kukausha majani yake na utwange au usage mashineni upate unga wake lakini bado juisi freshi ndiyo itakupa matokeo mazuri zaidi.

Labels:

Friday, April 13, 2018

Wanasayansi wagundua aina mpya ya chandaru


Wanasayansi wagundua aina mpya ya chandarua kinachoimarisha kinga dhidi ya Malaria


Kila mwaka takriban watu nusu milioni hufariki kutokana na Malaria. Suluhu moja rahisi ni kutumia vyandaruwa vya kujikinga na mbu vilivyotibiwa na viuatilifu vinavyoua vidudu.

Lakini kadri miaka inavyosogea, kumezuka tatizo jipya. Mbu wameweza kupambana na makali ya kemikali.

Wanasayansi wamepata suluhu, wamegundua kwamba vyandarua hivyo vikitumika pamoja na dawa ya viuatilifu (inayoua vidudu) inayojulikana kama Piperonyl Butoxide, inazuia mbu kuweza kupambana na viuatilifu, na hivyo kupunguza maambukizi ya malaria kwa zaidi ya theluthi moja.

Dkt Natacha Protopopoff, aliyeongoza majaribio ya aina mpyaya chandarua waliogundua ina iwezo wa kuimarisha kinga dhidi ya Malari, ameiambia BBC kwamba huenda neti hizo zikapunguza kwa kiwango fulani viwango vya ugonjwa wa Malaria.

"Majaribio haya ya aina hii mpya ya neti yanadhihirisha kupungua vizuri kwa maambukizi ya malaria.

Ilipunguza viwango kwa 44% katika mwaka wa kwanza, na pia 33% katika mwaka wa pili kwasababu vyandarua vimetibiwa kiwandani na hivyo kuruhusu kemikali hiyo kusalia katika chanadarua kwa miaka mitatau au kutumiwa katika majaribio."



Ugunduzi huo umefanywa na timu kutoka taasisi ya London School of Hygiene and Tropical Medicine, katika utafiti wao walioufanya kwa miaka miwili uliohusisha zaidi ya watoto elfu 15 nchini Tanzania.

Shirika la Afya duniani kwa sasa linashauri matumizi ya vyandarua hivyo vipya.
Mambo 10 kuhusu Malaria:
  • Malaria husababishwa na vimelea vinavyosambazwa baada ya mbu walioambukizwa navyo kuwauma binaadamu
  • Takriban nusu ya idadi ya watu duniani wamo katika hatari ya kuugua malaria
  • Watoto walio chiniya umri wa miaka 5 wamo katika hatari kubwa ya kuugua malaria
  • Viwango vya watu wanaokufa kutokana na malaria vinapungua
  • Kutambua na kutibu mapema wagonjwa wanaougua Malaria kunazuia vifo
  • Wasiwasi unaongezeka kuhusu uwezo wa vimelea kupambana na makali ya dawa za kutiba malaria - artemisinin
  • Kulala chini ya vyandarua vilivyotibiwa vya kujikinga na mbu, kunakinga maambukizi ya malaria
  • Kupuliza dawa ndani ya nyumba ndio njia muafaka ya kupnguza haraka maambukizi ya Malaria
  • Wanawake waja wazito ndio wako katika hatari kubwa ya kuambukizwa malaria
  • Malaria inasababisha athari kubwa kiuchumi katika nchi maskini



Matokeo yanapokelewaje Tanzania..

Matokeo ya utafiti huu yamechapishwa katika jarida la afya la Lancet.

Matokeo yanayoonekana kuwa mazuri ya majaribio ya vyandarua hivi Tanzania tayari yamechangia shirika la afya duniani WHO kupendekeza vitumiwe pakubwa.

Dkt. Govella is Mwanasayansi mkuu wa utafiti na mkuu wa idara ya utafiti wa Malaria katika Taasisi ya Afya Ifakara, anasema:

Nina matumaini kwamba vyandarua vinavyojumuisha kemikali stahili (piperonyl butoxide) iliyogunduliwa hivi karibuni vitatusaidia kuendeleza kazi nzuri iliopo sasa kutokana na matokeo ya matumizi ya vyandaruwa vilivyotibiwaDkt Nico Govella, Mwanasayansi mkuu - Taasisi ya Afya Ifakara Tanzania

"Uwezo wa mbu kupambana na makali ya viuatilifu vinavyotumika katika vyanarua umekuwa ni changamoto kubwa katika vita vya kupambana na malaria duniani.

Nina matumaini kwamba vyandarua vya kujikinga na mbu vinavyojumuisha kemikali stahili (piperonyl butoxide) iliyogunduliwa hivi karibuni vitatusaidia kuendeleza kazi nzuri iliopo sasa kutokana na matokeo ya matumizi ya vyandaruwa vilivyotibiwa."

Matumizi ya vyandaruwa vilivyotibiwa vya kujikinga na mbu imesaidia kupunguza idadi ya vifo vya malaria kwa miaka kadhaa, lakini hatua zimekwama hivi karibuni katika kupambana na ugonjwa huo.

Source: Click Here

Labels:

Thursday, April 12, 2018

Ccbrt na Tcco Waendesha Mafunzo ya Matibabu ya Nyayo za Kupinda


Ccbrt na Tcco Waendesha Mafunzo ya Matibabu ya Nyayo za Kupinda

Mmoja wa wataalamu akitoa huduma kwa mtoto mwenye nyayo iliyopinda kwa kutumia njia ya Ponseti katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam.
Wataalamu wakiendelea kutoa huduma kwa wtoto wenye nyayo zilizopinda kwa kutumia njia ya Ponseti katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam.
Excutive Director Miracle Feet, Chesca Colloredo akizungumza jambo.


HOSPITALI ya CCBT ya Jijini Dar es Salaam kwa kushirikiana na Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojishughulisha na kutoa huduma na matibabu ya nyayo za kupinda Tanzania( TCC0) wameendesha mafunzo ya wiki moja ya namna ya kutibu nyayo zilizopinda.

Huduma hiyo iliandaliwa pia kwa kushirikiana na wadau wa mradi wa mafunzo ya matibabu ya nyayo zilizopinda Afrika (ACT).
Mwenyekiti wa TCCO, Dkt. Robert Mhina akizungumza jambo.


Mafunzo hayo yanalengo la kujenga uwezo katika utoaji wa matibabu wa nyayo za kupinda ukanda wa kusini mwa jangwa la sahara kwa kutumia njia ya Ponseti, njia ambayo matibabu hutolewa bila kufanyika upasuaji.

Jumla ya washriki 65 wameshiriki mafunzo hayo wakiwemo wakufunzi maarufu wa matibabu ya nyayo zilizopinda duniani na wale wa kozi ya juu ya matibabu ya ulemavu huo, pia yametolewa mafunzo ya awali kwa wanaoanza kujifunza utaalamu huo.

Katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo, Ofisa Mwendeshaji wa CCBRT, Brenda Msangi aliwakaribisha washiriki hao Tanzania, na kusema kuwa mafunzo hayo ni fursa ya pekee kwa CCBRT katika kuwaendeleza wataalamu wake wa ndani na hatua muhimu ya kujiimarisha kama kitovu cha mafunzo ya afya katika eneo la Afrika Mashariki.


“ Ili kuhakikisha idadi ndogo ya wataalamu wa afya walioko hapa nchini wanajengewa uwezo na nyenzo wanazozihitaji kutoa huduma bora kwa wagonjwa. CCBRT imeanzisha kituo cha mafunzo ya afya hapa Dar es Salaam na kitakuwa na mazingira ya hali ya juu ili kuwapatia ujuzi unaostahili wauguzi na wataalamu wengine wa afya,” alisema Brenda.

Kwa upande wake mmoja wa Madaktari Bingwa wa Upasuaji Mifupa CCBRT Dkt. Prosper Alute aliwataarifu washiriki wa mafunzo hayo akisema kuwa takribani watoto 2,200 Tanzania huzaliwa na nyayo za kupinda kila mwaka.


“CCBRT ni mtoaji mkubwa wa matibabu wa nyayo za kupinda hapa nchini na idara yetu ya mifupa inaowataalamu waliobobea katika kutoa matibabu ya nyayo zilizopinda kwa kutumia njia ya Ponseti na hii hutuwezesha kutibu watoto kama 400 hivi kwa mwaka . Lakini idadi hii bado ni ndogo ikilinganishwa na watoto wenye mahitaji, mafunzo kama haya yatasaidi kuziba pengo. Alisema Alute.


Aidha aliongeza kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kuendelea kufanyika katika Bara la Afrika ambapo inakadiriwa kuwa watoto wapatao 30, 000 wanazaliwa na nyayo zilizopinda kila mwaka, huku kukiwa na wataalamu wachache wa kuweza kutoa matibabu hayo.

Labels:

Wednesday, April 11, 2018

Dodoma Yatajwa Kuongoza Kwa Ugonjwa wa Kipindupindu


Dodoma imetajwa kuongoza kwa idadi kubwa ya wagonjwa wa kipindupindu. Kati ya wagonjwa 1,448 wa nchi nzima, 583 wamepatikana mkoani humo

Ruvuma imeshika namba 2 kwa kuwa na kesi 374 sawa na 25%, Rukwa na Iringa ikiwa na kesi 276 sawa na 19%.

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Watoto na Wazee imeeleza kuwa Mkoa Manyara ndio wenye idadi ndogo ya wagonjwa wa kipindupindu. Kesi zilizoripotiwa ni asilimia 0.6 tu ya wagonjwa wote nchini.





Labels:

Thursday, March 22, 2018

Waziri wa Afya Atoa Tahadhali kwa Wananchi


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu amewashauri wananchi kwenda vituo vya tiba haraka mara baada ya kugundua kuwa wana dalili za ugonjwa wa dengue.

Tokeo la picha la Ummy Mwalimu

Hayo ameyasema wakati alipotoa tamko juu ya kuingia kwa ugonjwa wa dengue hapa nchini mara baada ya kufunga Mkutano wa 65 wa Jumuiya ya Mawaziri wa Afya wa Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini ECSA leo jijini Dar es salaam.

“Kuna dalili za Ugonjwa Dengue zikiwemo homa ya ghafla, kuumwa kichwa hususan sehemu za macho, maumivu ya viungo na uchovu. Dalili hizi huanza kujitokeza kati ya siku 3 hadi 14 tangu mtu alipoambukizwa virusi vya homa ya Dengue hivyo Wizara inashauri kuwa wananchi wasiwe na hofu, bali mara tu wanapoona dalili za ugonjwa waende katika vituo vya tiba" amesema Waziri Ummy.

Aidha Waziri Ummy amesema kuwa wakati mwingine dalili za ugonjwa huo zinaweza kufanana sana na dalili za malaria hivyo wananchi wanaaswa kwamba, wakipata homa wahakikishe kuwa wanapima ili kugundua kama wana vimelea vya malaria au Dengue, au sababu nyingine, ili hatua stahiki zichukuliwe.

Waziri Ummy amesema kuwa ili kujikinga na ugonjwa huo ni lazima Kuangamiza mazalio ya mbu kwa kufukia madimbwi ya maji yaliyotuama au nyunyuzia dawa ya kuua viluwiluwi vya mbu kwenye madimbwi hayo pamoja na Kujikinga na kuumwa na mbu kwa kuvaa nguo ndefu muda wote hasa nyakati za mchana.

Labels: