Monday, May 7, 2018

Hatimaye Nchi ya Saudi Arabia yaruhusu Ujenzi wa Makanisa Baada ya Katazo la Muda Mrefu


Hatimaye Nchi ya Saudi Arabia yaruhusu Ujenzi wa Makanisa Baada ya Katazo la Muda Mrefu




Nchi ya Saudi Arabia imeamua kuruhusu ujenzi wa makanisa baada ya kusainiwa kwa makubaliano kati ya viongozi wa Wahhabi na Kadinali wa Vatican.

Makubaliano hayo kati ya Rais wa Baraza la Kipontifiki ya midahalo ya dini mbalimbali, Kadinali Jean-Louis Tauran na Sheikh Mohammed bin Abdel Karim Al-Issa, ambaye ni Katibu Mkuu wa NGO kubwa ya Wahhabi yanalenga kuruhusu ujenzi wa makanisa pamoja na mikutano ya Waislamu na Wakristo mara moja kila baada ya miaka miwili.

Saudi Arabia ni moja ya nchi zisizo na uvumilivu kwa dini nyingine zaidi ya Uislamu. Wasio waislamu wanaadhibiwa kwa kuonesha matendo ya dini yao nje ya nyumba zao huku Muislamu yeyote anayeamua kubadili dini akihukumiwa kifo. Sheria za kiislamu zinawahusu wote wanaoishi nchini humo bila kuzingatia imani zao huku Jeshi la Polisi likisimamia ufuatwaji wake.

Hadi sasa inakadiriwa kuwa kuna Wakristo zaidi ya Milioni 1.5 nchini humo ambao ni wahamiaji wanaofanya kazi hususani kutoka nchi ya Ufilipino.

Uwezekano wa ufanikiwa kwa harakati hizi za Vatican zilizoanza mwaka 2008 ulianza kuonekana baada ya Mwanamfalme Mohammed bin Salman kuingia madarakani ambapo amedhamiria kubadili muonekano wa nchi hiyo kimataifa kwa kubadili mambo kadhaa.

Katika kipindi chake tayari ameshabadili taratibu kadhaa zilizokuwepo kwa miaka mingi kama wanawake kutoruhusiwa kuendesha magari na kutakiwa kuwa na mwangalizi muda wote.

Labels:

Monday, April 16, 2018

Muhubiri Dar afunguka kuhusu kutoza malipo


Muhubiri Dar afunguka kutoza malipo kwa kila anaetaka kuombewa na yeye


Prophet Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM Kivule Dar es salaam amefunguka kuhusu taarifa za yeye kulazimisha kila Mtu anaetaka kuombewa na yeye kulipia maombezi hayo kwa lazima kanisani kwake Kivule Dar es salaam.

Phrophet Suguye ameongea na millardayo.com na AyoTV na kusema kilichotokea ni kwamba aliomba Watu wanaokwenda kuombewa nae kuchangia pesa kwa ajili ya kuanzisha TV ya kanisa iitwayo WRM ambayo inapatikana STARTIMES na kwenye AzamTV, hivyo hakulazimisha.

“Nilisema wale wanaotaka kuja kuombewa kwenye ibada kanisani iliku bure kabisa lakini kwa waliotaka kuniona wenyewe ofisini kwangu ndio nilisema wachangie TV, hata hivyo hakuna tena huo utaratibu wa kuchangia TV, hiyo laana ya kutoza watu pesa kwa maombezi sina” – Nicolaus Suguye


Labels:

Thursday, April 5, 2018

Majambazi Wavamia Kanisa Katoliki Mbezi


Majambazi Wavamia Kanisa Katoliki Mbezi na Kupora Fedha na Vifaa vya Kuendeshea Misa


Majambazi wamevamia na kuvunja kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu-Mbezi Mwisho jijini Dar es salaam, na kupora fedha na vifaa vya kuendeshea misa.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam, Lazaro Mambosasa, amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo, ambapo majambazi hao waliingia kanisani hapo na kuiba vitu hivyo, ikiwemo fedha za sadaka zilizokusanywa tangu sikukuu za pasaka mpaka sasa.

“Ni kweli nimepokea simu kuwa kuna hilo tukio, ni vibaka wameingia hapo kanisani na kuiba pesa na baadhi ya vitu, pesa ambazo zilikuwa za sadaka tangu sikukuu, ila thamani yake bado hatujaijua kwa sababu ndio tukio limeripotiwa sasa, baada ya muda nitakuwa na taarifa kamili”, amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema jeshi la Polisi linafanya uchunguzi kuwabaini waliohusika na tukio hilo, ili kuwafikisha mbele ya sheria.

Labels:

Thursday, March 22, 2018

The Life of Muhammad


Just like the life of Jesus, whether you are a follower of Muhammad (570-630) or not, you cannot deny the impact his life has had on history. Before Muhammad rose up as the founder of Islam, the Middle East was full of small tribes that warred against each other continuously. Muhammad brought those tribes together and gave them a purpose and a reason to join forces. Though blood was still shed, it was not against each other. It was against those that threatened the new religion or fought against it.


After Muhammad brought together the Middle East, the region experienced the Islamic Golden Age from 786 to 1258 AD. This time is analogous to Europe's Renaissance (though during this time, Europe was still in the Dark Ages). The region's culture flourished and made many advances in fields including mathematics and science. The world benefited from Muslims' discovery of the immune system, preservation of Roman and Greek texts, and invention of the number zero, the decimal system, and algebra. Even coffee was discovered during the Islamic Golden Age! The stability Muhammad brought to the region was one of the reasons that the culture was able to make such advances.

Since the birth of Islam, it has become one of the largest religions of the world. It covers the globe, and through many of its sects, it has influenced the world. The terrorist branches have reached out and impacted the daily lives of every person through their traveling procedures or just the way they go to work with extra security. Muhammad changed the shape of the Middle East that is still changing today.
Muhammad directing Black Stone
Muhammad
Mosque by Steve Evans on wikimedia commons
Qu'ran by Amr Fayez on wikimedia commons



Labels:

Adhana Imepigwa Marufuku Kigali Rwanda, Inasumbua Wananchi

Marufuku ya matumizi ya adhana{ Wito kwa Waislamu kuhudhuria maombi} katika tarafa moja ya mji wa Kigali nchini Rwanda imepingwa vikali na baadhi ya Waislamu jijini humo.

Tokeo la picha la MOSQUE

Utawala katika tarafa ya Nyarugenge kunakopatikana jamii kubwa ya Waislam nchini humo umebainisha kuwa kumekuwepo muafaka wa kubadili mbinu za kuwaita waumini bila ya matumizi ya njia hiyo ambayo inatajwa kuwasumbua wananchi.

Kulingana na taarifa kutoka Kigali Waislamu kuhudhuria maombi umetajwa kuwa kero miongoni mwa wananchi.

Tayari mkataba wa kuhakikisha kuwa mwafaka huo unaheshimiwa umetiwa saini kati ya viongozi wa msikiti na utawala wa eneo hilo.

Wito huo wa maombi miongoni mwa jamii za Waislamu kote duniani hutumia vipaza sauti na hufanyika mara tano kwa siku.

Licha ya utawala wa eneo hilo kudai kwamba kumekuwa na mwafaka kutoka pande zote mbili baadhi ya Waislamu waliohojiwa wametoa hisia tofauti.

Kulingana na katibu mtendaji wa tarafa hiyo ya Nyarugenge, amri hiyo iliagizwa yapata miaka maiwili iliopita lakini ikapuuziliwa mbali.

”Pengine wakati ule sababu ambazo watu hawakupokea vyema ujumbe ilikuwa hakuwa umeelezewa sawa sawa ,lakini leo baadhi ya makanisa yalilazimika kufunga milango baada ya kushindwa kutimiza kanuni za ujenzi huku misikiti yenye vipaza sauti na makanisa yenye kengele tukiyataka kutotumia mtindo huo. Mtu aliye lala akiishi jirani na kengele hiyo inampigia kelele. Kwa hiyo ni uamzi unaohusu pande zote nna ni matarajio yetu kuwa hakuna aliyenyimwa haki.”

Naye mshauri wa Mufti wa Rwanda shekh Mbarushimana Suleinam alisema kuwa hatua hii ya kuzuiliwa kwa matumizi ya adhana misikiti inafuatia operesheni inayoendela ya kufungwa kwa makanisa na vigango Zaidi ya mia saba ambavyo viliripotiwa kuwa havijatimiza kanuni za ujenzi na amri ilitolewa kwanza kutimiza matakwa ili zipewe tena idhini ya kufanya kazi.


Labels:

Friday, March 9, 2018

Nabii Olivia Asikika Akimpanga Muumini Apige Kelele


Kweli siku za mwisho zimekaribia, Shuhudia katika Video Nabii Olivia wa




Kanisa la Repohim Church amesikika akimpanga muumini apige kelele akiashiria mapepo yanamtoka.

Tazama Video Hapa Chini:

Labels:

Tuesday, February 13, 2018

MAISHA HATIMAYE: DAY 2

Huu ni muhtsari wa mahubiri ya MAISHA HATIMAYE yanayoendelea Jijini Mbeya pia yanarushwa live kupitia Morning Star Tv na Radio yakiletwa kwenu na Chama cha Wajasiriamali na Wanataaluma Waadventista nchini Tanzania (ATAPE) huku mnenaji akiwa ni Makamu wa Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana toka nchini Marekani.




"DHAMANA YA THAMANI KUU"
WIMBO: MAISHA HATIMAYE (GOSPEL FRIEND)
 Dhamana ni kitu ambacho ni cha thamani kubwa na umepewa ili ukitunze maana si chako.

- Kitu cha thamani Kubwa Mno Kuliko kitu kingine chochote chini ya Jua.

- Wakati Mwingine kupewa kitu cha thamani kunakufanya uwe wa thamani pia. Na hivyo inatakiwa ukitumie kwa uthamani wake pia.

- Kupewa kitu cha thamani ni Kuaminika, kuheshimika, kupendwa na inahitaji kuurudisha upendo kwa namna ya pekee.

- KUNA KAWAIDA AMBAYO SI YA KAWAIDA.

Karne ya 21 inafanya mambo flani ya kawaida sana lakini sio ya kufanya kawaida kama wanavyoyafanya.

-LEO KUUA IMEKUWA KAWAIDA LAKINI SI, KAWAIDA-
  •  Tangu vita vya kwanza vya Dunia watu wanauana na kuuana imekuwa kawaida lakini SI KAWAIDA.
  •  KAMA HALI INAENDELEA KUWA HIVI NA DUNIA IMEJAA VIFO 
Swali: JE, MAISHA YA MWANADAMU YANA THAMANI GANI SASA?

JE, MAISHA NI NINI?
- Wengine Maisha mazuri kwao, ni kupata Gari, Nyumba, Pesa na vitu vingine vya Thamani sana. Lakini Je, maisha Ya Thamani/ Maisha Mazuri Ni Nini?
- Maisha si mali, maisha si kutafuta Pesa, Maisha si kuwa na Nyumba na vitu vya Samani ndani Yake. (KUMBE VITU/ MALI KAMWE SI MAISHA). 
- Mali inaweza ikakupumbaza na kukufanya uifanye kuwa maisha lakini vyote hivyo ni ubatili.
- Wengine husema maisha ni Maadili ya Dini..


Je, Haya Maisha Yanatoka wapi?

- Maisha ni uhai  unavyoutumia huo uhai. Jambo la Msingi ni hili;

Hakuna Maisha Bila Uhai.

- Haupatikani mahali popote duniani, hospitali, dukani, maabara, sokoni wala mahali popote. Je, unapatikana wapi sasa huo uhai?

- Mungu amejifunua katika maandiko kwa namna ya ajabu sana na alimtoa mwanawe wa pekee ili aje duniani akautoa uhai wake.

- Mungu wetu aliumba na kutoa uhai kwa Viumbe vyote vilivyoko duniani. Wanyama, ndege, mimea na kila namna ya vitu vyote viendavyo kwa uhai.

- Siku ya Sita alimuumba mwanadamu kwa Mfano Wake.

Maisha yako yasiharibiwe na vitu ambavyo ukivitazama vinakufanya uwe na majonzi, vinavyokuhabia furaha yako... VIKO VITU VINGI AMBAVYO MUNGU ALIUMBA VYA AJABU NA KUPENDEZA, KAA NAVYO NA MAISHA YAKO YATAKUWA NA FURAHA SIKU ZOTE.

Zipo Nadharia Nyingi zinazoelezea namna ambavyo dunia hii ilitokea. Lakini Leo Kataa kwa sababu wewe una thamani kuu mbele za Mungu.

ALIKUUMBA KWA MFANO WAKE NA AKAKUPATIA PUMZI YA UHAI.

MUNGU AKUONGOZE KATIKA KULITAMBUA HILI. LEO NAKUTANGAZIA WEWE KUWA

KILA MWANADAMU ALIYE CHINI HAPA DUNANI LEO NA AUTHAMINI UHAI AMBAO MUNGU AMEMPATIA. KUTOKA KATIKA SURA NA MFANO WAKE..

MUNGU ANAKUTHAMINI MNO. THAMINI UHAI ALIOKUPA..

Wimbo: Namba 5-Na Tumwabudu Mfalme Mtukufu


MUNGU AKUBARIKI SANA





Imeandaliwa na;
MALIMA, K.

Labels:

MAISHA HATIMAYE: DAY 1


Huu ni muhtsari wa mahubiri ya MAISHA HATIMAYE yanayoendelea Jijini Mbeya pia yanarushwa live kupitia Morning Star Tv na Radio yakiletwa kwenu na Chama cha Wajasiriamali na Wanataaluma Waadventista nchini Tanzania (ATAPE) huku mnenaji akiwa ni Makamu wa Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Ulimwenguni Mchungaji Geofrey Gabriel Mbwana toka nchini Marekani.



KISIMA KISICHOKAUKA: MUNGU NI MKUU
  •   Haya ya Maji na kiu inapotokea hutaabisha sana. Na ikiwa hakuna maji kiu hutaabisha.
  •  Uhaba wa Maji ni dhiki, taabu na pia ni kiu mbaya.
  • Ikiwa hata kuna kiu Kali, lakini kuna kisima cha Maji Kisicho kauka.. Maisha huwa ni mazuri
  • Pengine umepitia ukame na Jangwa katika maisha na unatafuta njia pekee ya Kutoka katika taabu yako(kiu yako).. Leo kipo kisima kisicho kauka. 
  • Ukikipata na ukakitumia kwa makusudi Yaliyowekwa utashuhudia Makubwa Kwa Maisha Yako. Na hautaona kiu Tena.
ZABURI 36:9

- Maana Kwako wewe iko chemchemi Ya Uzima. Ambayo Ni Mungu Pekee aliye Chemchem Ya Uzima.

- Yesu amegusa maisha yako na ameugusa moyo wako leo ione chemchem ya uzima.

- Kuna watu wanatembea wakiwa wamekufa na hawaoni badiliko lolote katika maisha, wanahitaji uzima.

- Yesu Ndiye awezaye kukifunua kisima cha uzima ndani yetu na maji yakabubujika ndani Ya mioyo Yetu.

- Mungu Ni Mkuu Mno, ana majina mengi sana maana na yanatumika haya mengi kwa Sababu Ya sifa zake.

- Wakati Mwingine tumemfanyia matani, tukamshusha kwa ngazi zetu za Kibinadamu tukamuweka kwa viwango vya chini sana...lakini Leo nakutangazia MUNGU NI MKUU MNO


YEREMIA 10:6

- Wewe Mungu ni Mkuu Mno, Jina Lako Ni Kuu, Wewe mwenyewe ni mkuu na Mungu wako Ni Mkuu.

1 Nyakati 16:5

- Hakuna Mungu Kama wewe, hakuna wa kulinganishwa kama wewe

- Muache Mungu aitwe Mungu, na Ni Mkuu katika Mambo Haya;

1) UMBILE LAKE - Halielezeki

2) UWEZO

3) SIFA ZAKE (Ni hizi) nazo ni za peke Yake
  •   KWA MAMLAKA
  • NI WA MILELE 
  • ANAJUA YOTE 
  • HABADILIKI BADILIKI 
  • NDIYE MWENYE UWEZA WOTE 
  • SI WA KUFANYIWA MZAHA 
  • NI WA KUTISHA TENA SANA 
  • NI MUNGU MWENYE UPENDO, MPOLE, REHEMA, MVUMILIVU, FADHILI. 


" ANASHUKA AINGIE KATIKA MAISHA YAKO."

Anashuka Ili Akupandishe Juu akuweke Kifuani Mwake, Mkaribishe akubariki na kukuweka kifuani mwake. Akishuka mpokee, mkaribishe na mpe Nafasi.

Mwanzo 28:15

- Mungu huyu aliye Mkuu anajali Sana Maisha Yako, anakufaham na anajua kila kitu kuhusu wewe.

- Tazama mimi nipo pamoja nawe Leo Hii Tambua..UPO KWENYE UWEZA WA MUNGU....

- Anatembea pamoja na wewe ukimkubali, na ukimkataa anatembea pembeni yako anakulinda na kukuwekea Ulinzi.

- MUNGU ANAKUPENDA YUKO MAISHA MWAKO NA ANANGOJA UWEKE MAHUSIANO YA DHATI PAMOJA NAE..

Ayubu 22:11

- Kama tunataka mema maishani mwetu, MJUE SANA MUNGU, MEMA YATAKUTOKEA.

- Mtafute anapatikana, mchunguuze utamuona na mtafakari atakutokea. MUNGU WETU NI MKUU


ISAYA 40:26

- Mungu ni Mkuu anajua majina ya kila nyota.. Ni ukuu wa namna gani Huu...ajabu sana Mungu wetu Ni Mkuu...mamilioni ya Nyota aliyaumba na kuyawekea namna ya mzunguko wake. Na ajabu anaziita kwa majina.

Msaada wangu utatoka wapi? Unapatikana kwa Mungu Pekee, Mkabidhi Maisha Yako Leo.

Wimbo: Namba 7: Mungu Msaada Wetu

BWANA AKUBARIKI SANA. 
Imeandaliwa na;
MALIMA, K.

Labels: