Thursday, April 5, 2018

Mji wa kale wa zaidi ya miaka 5,000 wagunduliwa Misri


Mji wa kale wa zaidi ya miaka 5,000 wagunduliwa Misri

Haki miliki ya pichaEGYPTIAN MINISTRY OF ANTIQUITIESImage captionMji huo huenda ulikuwa makao ya wachimbaji na wajenzi wa makaburi

Wanaakiolojia nchini Misri wamegundua kile wanachosema ni mabaki ya mji ambao ulikuwepo zaidi ya miaka 5,000 iliyopita.

Wamepata nyumba, vifaa, vyungu na makaburi makubwa.

Mabaki hayo yamo eneo la ukingo wa mto Nile, karibu na hekalu la Seti, eneo la Abydos.

Wataalamu wanasema makaburi 15 yaliyogunduliwa yanaashiria kwamba ni watu wa hadhi ya juu waliozikwa humo.

Mabaki ya Wafilisti yapatikana Israel

Inaaminika kwamba mji huo ulikuwa makao ya maafisa wakuu wa serikali na wachimbaji na wajenzi wa makaburi, ambao ulifana enzi za kwanza kabisa za Misri ya kale.

Wataalamu wanasema ugunduzi huo huenda ukasaidia kufufua sekta ya utalii nchini humo ambayo imeathirika pakubwa kutokana na machafuko yaliyofuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Hosni Mubarak mwaka 2011.

Haki miliki ya picha EGYPTIAN MINISTRY OF ANTIQUITIES Image caption Picha inaonesha kile ambacho wataalamu hao wanasema ni makaburi yaliyogunduliwa katika mji huo

Wanaakiolojia wanasema wamegundua vitu vingi kwenye mji huo vikiwemo majumba, vigae vya vyungu na vifaa vilivyoundwa kwa kutumia chuma na mawe.

Lakini mtathmini wa BBC wa masuala ya Mashariki ya Kati Alan Johnston anasema muhimu zaidi ni makaburi yaliyogunduliwa.



Inaaminika kwamba maafisa wakuu na wajenzi wa makaburi, ambao huenda walihusika katika kujenga makaburi ya kifalme katika mji mtakatifu wa Abydos hapo karibu waliishi eneo hilo. Mji wa ABydos una mahekalu, na unaaminika kutumiwa kama mji makuu wakati mmoja enzi za kale za utawala wa Misri.Haki miliki ya picha EGYPTIAN MINISTRY OF ANTIQUITIESImage captionBaadhi ya vitu vilivyogunduliwa eneo ambalo wataalamu wanasema kulikuwa an mji zaidi ya miaka  5,000 Haki miliki ya picha GETTY IMAGES Image caption Maeneo ya akiolojia karibu na Luxor (pichani) na kwingineko Misri yametatizika kuwavutia watalii kutokana na misukosuko ya kisiasa

Labels:

Mabaki ya binadamu wa kwanza yapatikana Morocco


Mabaki ya binadamu 'wa kwanza' yapatikana Morocco

Haki miliki ya pichaPHILIPP GUNZ/MPI EVA LEIPZIGImage captionUjenzi wa kwanza wa kisukuku cha awali zaidi cha binadamu kutoka Jebel Irhoud (Morocco) kulingana na nakala za tomografia.

Uchunguzi umebainisha kuwa dhana ya kuwa asili ya binadamu wa kwanza ni kutoka Afrika ya Mashariki zaidi ya miaka laki mbili iliyopita sio kweli.

Visukuku vya binadamu watano wa mapema imepatikana Kaskazini mwa Afrika na inaonyesha binadamu wa kwanza aliishi miaka 100,000 zaidi ya vile ilivyodhaniwa.

Prof Jean-Jacques Hublin, kutoka Leipzig, Ujerumani, anasema kuwa ugunduzi huu unaweza "kuandika upya vitabu vya kiada" kuhusu kuibuka kwetu .

"Sio hadithi ya hayo kutokea kwa njia ya haraka katika 'shamba la Edeni' mahali fulani barani Afrika. Ilikuwa ni maendeleo ya taratibu. Kwa hiyo kama kulikuwa na bustani ya Edeni, ilikuwa ni kote kote Afrika.

"Mji wa kale sana wagunduliwa Misri

Binadamu wa kale huenda 'hawakuishi zamani sana'

Prof Hublin alikuwa akiongea katika mkutano wa wanahabari katika chuo kimoja mjini Paris, ambako aliwaonyesha waandishi kisukuku ambacho timu yake ilichimbua katika eneo la Jebel Irhoud, Morocco. Sampuli hiyo ni ya na fuvu, meno na mifupa mirefu.

Mabaki yaliyopatikana katika eneo hilo hapo awali yalisemekana kuwa na miaka elfu 40. Lakini Prof Hubli alikuwa na tashwishi na kwa muda mrefu aliendelea kufanya utafiti katika eneo hilo la Jebel Irhoud na miaka 10 baadaye, anawasilisha ushahidi mpya unaoelezea hadithi tofauti.
Nyayo za wanadamu wa kale zagunduliwa Tanzania

Mabaki hii ya sasa inadaiwa kuwa na umri wa kati ya miaka 300,000 na 350,000 miaka. Na fuvu yake ni ya aina karibu sawa na ya binadamu wa kisasa.

Hadi sasa, mabaki ya binadamu wa kwanza yalikuwa kutoka Ethiopia (kutoka tovuti inayojulikana kama Omo Kibish) , Afrika mashariki na walidaiwa kuwa na umri wa takribani miaka 195,000.
Ushahidi wa zamani kuhusiana na maisha 'wapatikana'

Kabla ya watu wa aina yetu, kulikuwa na aina nyingi tofauti ya binadamu, na kila alikuwa na uwezo na udhaifu tofauti. Na hawa aina mbalimbali ya binadamu, kama vile wanyama wengine, waliendelea kubadili muonekano wao hatua kwa hatua.

Jebel Irhoud inafanana na sehemu kadhaa za kihistoria barani Afrika ambayo ina miaka 300,000. Maeneohaya yana zana sawa na pia ushahidi wa matumizi ya moto.

Labels:

Monday, April 2, 2018

Meli ya abiria ya Uingereza iliyozamishwa mwaka 1942 yaibuliwa baharini


SS Sagaing: WW2 shipwreck re floated by Sri Lanka navy

Image copyright SRI LANKA NAVY Image caption Divers from Sri Lanka's navy had to reinforce the vessel's frame before raising it

A British passenger ship that sank after it was bombed in a Japanese air strike in World War Two has been raised off the Sri Lanka coast after 75 years.

The SS Sagaing, whose passengers and cargo were largely saved back in 1942, has been refloated with the help of a team of divers from Sri Lanka's navy.

It had been resting about 35ft (10.7m) under the water at Trincomalee harbor.


The salvage operation took several months and was carried out by Sri Lanka's Eastern Naval Command unit.Image copyright SRI LANKA NAVY Image caption The operation to bring the wreck to the surface took several months

It required the strengthening of the 452ft long vessel's main structural framework, which began on 11 September 2017, Sri Lanka's navy said in a statement on Saturday.

The team of divers also erected an artificial side to the ship in order to seal an area before "dewatering" it to recover lost buoyancy. Stunning pictures of Black Sea shipwrecks


Prior to the ship's refloat, the damaged sunken vessel was used as a pier for other naval ships in the harbour. Image copyright SRI LANKA NAVY Image caption The SS Sagaing before the Japanese bombing

Labels:

Thursday, March 8, 2018

Wajue Waliogundua Umeme


Pata picha dunia ya leo kusiwe na umeme,Dunia ingekuaje? maisha yetu yangekuaje?,je watu wangetambua tabia za sayari nyingine huko anga za juu?Vipi tungezijua simu?Vipi tungetumia kompyuta,intaneti? ni wazi pangekuwa panaboa (bore) sana.
Katika ulimwengu wa sasa watu wengi sana wanatumia umeme katika kuendesha shughuli mbalimbali,na wengine hawawezi kufikiri katika maisha yao bila ya kuwapo kwa umeme.

Japo tunafahamu kuwa umeme ni nishati inayozalishwa na tabia asili ya mazingira ila iliwachukua miaka mingi sana binadamu kujua jinsi ya kuutumia umeme ili kuendesha vitu vingine mfano taa na injini.
Swali la kwamba 'nani aligundua umeme ?' limekuwa gumu kujibu kwa neno moja au kwa kumtaja mgunduzi mmoja,kwakuwa wagunduzi ni wengina kila mmoja alikuwa na umuhimu wake katika ugunduzi huo.Ugunduzi wa umeme ni historia ilio kubwa na 'vichwa' vingi vilitumika katika kukamilisha ugunduzi huu.

Angalau tu kwa ufupi,tuangazie wale walioshiriki katika ugunduzi huo japokuwa ilikuwa katika miaka tofauti.

Mambo ya mwanzo kabisa yaliofanyika ambapo matokeo yake ni haya tunayaona leo,mfano tunapiga pasi kwa kutumia umeme,mambo haya yaliohakikisha mafanikio katika ugunduzi uliokuja kufanyika miaka ya baadae na akina BENJAMIN FRANKLIN na wengine yalianza katika miaka ya 600 BC.

Benjamin Franklin 

THALES wa MILETUS, alikuwa ni mwanasayansi wa mwanzo kutambua uwepo wa umeme katika mazingira ya asili.THALES alitambua 'mbegu' ya umeme tuli (STATIC ELECTRICITY) na kupendekeza nadharia ambayo ilieleza "Kusugua manyoya kutafanya kitu kuvuta kingine (kuvutana)" hapa unaweza kuielewa vyema nadharia hii kwa kufanya jaribio lifuatalo wewe mwenyewe.
UTAHITAJI;
  • Kitana
  • Vipande vidogo vidogo vya karatasi
  • Na manyoya lakini kama hukuyapata unaweza kutumia nywele za kichwani kwako.
HATUA;
  • Sugua manyoya au nywele za kichwani kwako kwa kutumia kitana ulichonacho (fanya hivyo kwa muda wa kama dakika moja tu) baada ya hapo,gusia juu ya vile vipande vidogo vya karatasi 
MATOKEO
  • Matokeo yake utaona vipande vya karatasi vinaganda kwenye kitana kama vyuma vinavyoganda kwenye sumaku.

THALES wa MILETUS

Mwanasayansi WILLIAM GILBERT ndie mtu wa kwanza kutumia neno 'UMEME' ,hii ilikuwa katika miaka ya 1600.

WILLIAM GILBERT

Katika mwaka 1660 OTTO VON GUERICKE aligundua kifaa cha kuzalisha umeme tuli (STATIC ELECTRICITY) ,ugunduzi wa kifaa hiki uliofanywa na bwana GUERICKE ulipelekea kutambulika zaidi kwa tabia za umeme au kwa maneno mengine tunaweza kusema ugunduzi wake uliwafunua watu ufahamu zaidi juu ya UMEME.Miongoni mwa tabia/sifa za umeme zilizogundulika ni-
  • Umeme unaweza kupita ndani ya 'vaccuum'
  • Katika muktadha wa umeme,kuna vitu/materials ya aina mbili,moja ni vile vilivyo na tabia ya kuruhusu umeme kupita na vinginevyo ni vile ambavyo haviruhusu umeme kuppita yaani INSULATORS na CONDUCTORS.
OTTO VON GUERICKE

Katika karne ya 17,karne muhimu zaidi katika ugunduzi wa vitu mbalimbali ikiwemo umeme,mwaka 1729 mwanasayansi STEPHEN GRAY alichangia katika uelewa zaidi wa umeme kwa kugundua uendeshaji wa umeme,miaka nane (8) baadae CHARLES FRANCOIS DU FAY aligundua kuwa umeme unaweza kuwa na elements aidha CHANYA (+) au HASI (-).
Baadae sasa mwanasayansi BENJAMIN FRANKLIN na EBENEZER KINNERSLAY walitoa majina kwa elements za umeme za HASI na CHANYA.Ugunduzi wa electro-magnetic induction ulieleza wazi ni kwa namna gani umeme uliweza kufanya kazi.
Tokeo la picha la STEPHEN GRAY
STEPHEN GRAY

Kwenye suala la electromagnetism,MICHAEL FARADAY alikuwa mtu muhimu sana kwa kuwa aligundua kuwa 'kupitisha sumaku katikati ya koili ya waya (WIRE COIL) kungeweza kuzalisha umeme; ni huyu huyu FARADAY ndie aliegundua injini/mashine inayoendeshwa kwa kwa kutumia umeme,baadae aliweza kutengeneza GENERATOR na TRANSFOMA (TRANSFORMER).

Tokeo la picha la CHARLES FRANCOIS DU FAY
CHARLES FRANCOIS DU FAY

Katika kipindi cha mwaka 1745-1747 ni PETER VAN MUSSCHENBROEK aliegundua 'LAYDEN JAR' ambapo ilikuwa na uwezo wa kuhifadhi umeme (STATIC ELECTRICITY) na kutoa kwa wakati huohuo.

> WILLIAM BENJAMIN
Mwanasayansi huyu aliamini kuwa 'radi ni mfumo wa umeme'
katika kuamini kwake huko hakuishia hapo,mnamo JUNE 15 1752,FRANKLIN alifanya jaribio ambalo ni maarufu sana la kurusha kishada wakati wa radi kwa lengo la kuthibitisha kuwa RADI ni mfumo wa umeme.
Kishada hiko alikifunga kitu cha asili ya chuma akiwa na lengo la kama kweli RADI ni mfumo wa umeme basi utapita kupitia kitu hicho cha asili ya chuma na kumfikia .
Kama zilivyo fikra zake,umeme kutoka kwenye RADI ulisafiri kupitia chuma kile na mpaka kumfikia bwana BENJAMIN FRANKLIN na kumpiga shoti.

LAKINI mwaka 1747 HENRY CAVENDISH alitoa orodha ya vitu vinavyopitisha umeme yaani materials that are conductive to electricity.Tukio hili lilifuatiwa na bwana VOCTA ambae yeye aliweka bayana kuwa 'chemical reactions'zinaweza kutumika katika kuzalisha 'anodes' na 'cathodes'
Ugunduzi wa BALBU(bulb) za umeme uliofanywa na THOMAS EDISON ilikuwa ni hatua kubwa sana katika maendelao ya teknolojia,na ni ilikuwa ni hatua ilioitoa dunia kwenye kiza.

Katika kipindi cha karne ya 20,umeme uliwafikia watu duniani kote,ugunduzi uliofanywa na wanasyansi tofauti tofauti na wagunduzi wa umeme kama akina THOMAS EDISON,SAMUEL MORSE na NIKOLA TESLA uliibadilisha kabisa dunia,dunia ya sasa kuna injini/mashine zinazotumia umeme kufanya kazi ambazo mwanzo zilikuwa zikifanywa na binaadam.
Wakati wa uhai wa wagunduzi akina THOMAS EDISON na WESTINGHOUSE kulikuwa na mabishano kati yao,mabishano hayo yalikuwa ni juu ya aina ya umeme uliofaa kutumiwa,THOMAS EDISON alipendekeza kutumika kwa umeme wa DIRECT CURRENT(DC) na WESTINGHOUSE yeye alipendekeza kuttumika kwa ALTERNATING CURRENT (AC).
Ugunduzi wao umetuletea manufaa makubwa, hivi sasa mitambo inagunduliwa kurahisisha kazi mitambo hiyo inategemea umeme kujiendesha,na hata teknolojia na tafiti za anga za juu zinakuwa rahisi kutokana na kuwepo kwa umeme. Hivi sasa umeme wa DC na AC wote unatumika ila tu hutegemea na mahali unapohitajika.

Reference CLICK HERE




Labels: