Jana Nilitafakari Nikagundua Age Yangu Na Kaka Zangu Wengine Imeenda Sana.
Tunazeeka Sasa, Niliona Mabantu Kwenye Interview Wanamuita Country Boi Kaka, Halafu Unakuta Mimi Country Ananiita Kaka Pia, Means Mabantu Wataniitaje Mm? Mm Namuita FID Kaka, Mabantu Watamuitaje FID? #Tunazeeka
Msanii mwanadada wa kizazi kipya Nandy anatarajia kuachia project yake mpya hivi karibuni.
Baada ya kupost twitter statement hii "tutoe project mpya nimewamiss", wadau walitiririka na kusema project wanaoisubiri ni kwa sasa kutoka kwake ni ndoa.
Ali Kiba Atamba "Sitegemei Kupata Pesa Kutoka Katika Views
Ali Kiba Atamba "Sitegemei Kupata Pesa Kutoka Katika Views za Youtube Kama Mnavyofikiria"
Msanii wa BongoFleva mwenye 'hit song' ya 'Mvumo wa Radi' Alikiba maarufu kama King Kiba amefunguka na kudai yeye sio miongoni mwa wasanii wanaotegemea kupata pesa kutoka katika 'views' za Youtube kama baadhi yao wanavyofikilia vichwani mwao.
King Kiba ametoa kauli hiyo ikiwa zimepita siku kadhaa tokea video yake mpya ya 'Mvumo wa Radi' kushindwa kuendelea kuhesabu idadi ya watu walioitazama jambo ambalo wengi wao walidai kuna kuna mchezo anafanyiwa msanii huyo ili asiweze kufikisha views wengi kama ilivyokuwa kawaida yake kila atowapo video.
"Hii ndio mara ya kwanza kunitokea tatizo hilo ila halijaweza kuniathiri kwa namna yeyote ile. Ila nashukuru watu wamepata walichokuwa wanastahili nasio kwamba mimi nategemea pesa kutoka 'Youtube views', mimi nafanya muziki najua wapi napata pesa katika muziki wangu. Nilichokuwa nahitaji kiukweli ni mashabiki zangu waridhike na waelewe mimi ni msanii wa aina gani", amesema Alikiba.
Pamoja na hayo, Alikiba ameendelea kwa kusema "tunajua kwamba kuna hizi biashara za kuweka ma-robot katika 'Youtube' ili ionekane watu wana 'view' kwa wingi ila mimi binafsi ninaona ni utoto tu. Haitokuja kutokea hata siku moja kwamba Alikiba ameweka 'robot' ili apate 'views' nyingi, mimi nafanya muziki wangu kwa ajili ya watu na kwanini sasa nidanganye watu". Wimbo wa Alikiba kwa sasa umetazamwa jumla ya watu milioni 1.2 na kushikilia nafasi ya kwanza katika ya video zilizotazamwa kwa kasi kubwa kutoka Youtube.
Ikiwa ni siku sita zimepita tangu Alikiba aachie ngoma yake mpya ‘Mvumo wa Radi’ amepokea tuzo ya heshima ya Plaque inayoitwa Nyota wa Mchezo kupitia kipindi cha The Playlist cha Times FM.
Msanii huyo amepewa tuzo hiyo juzi Jumatatu kutokana na mchango wake kwenye muziki na jitihada alizopiga kupeperusha bendera ya Tanzania na ku-wainspire wasanii wengine wachanga na kuendelea kuwepo mpaka leo kwenye muziki.
Kiba amekuwa msanii wa tatu kupewa tuzo hiyo baada ya Vanessa Mdee aliyekabidhiwa mwezi January mwaka huu na Diamond aliyepewa mwezi wa tatu.
Kwa sasa video ya ngoma yake mpya ya Mvumo wa Radi ina views milioni 1.1 kwenye mtandao wa YouTube.
Nahreel Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Kuhusu Rosa Ree
Nahreel Afunguka Kwa Mara ya Kwanza Kuhusu Rosa Ree Kutoka Lebo ya The Industry
Mtangazaji wa Wasafi Kipindi cha Refresh akimuhoji Nahreel kuhusu issue inayo endelea mtaani kuwa The Industry ilikuwa inambania Rosa Ree na Baada ya Kutoka katika Lebo hiyo inaonekana amepata mafanikio zaidi Nahreel amejibu hivi na kuweka mambo sawa :
" Nadhani Rosa Ree Watu Wamemjua Kupitia the Industry Kwahiyo hiyo ni tosha sisi tuliplay part yetu, na Kama Rosa alichokisema ilifika wakati ilibidi aendelee na mambo yake na sisi tukamlet aendelee na issue zake, sisi hatuna tatizo na Rosa Ree na hatujawahi kuwa na tatizo na mtu yoyote tuliplay part yetu na yeye anaplay part yake" Nahreel
Mama wa Jay-Z: Nilimwambia Mwanangu Nina Mpenzi wa Jinsia Moja
Mama yake mwanamuziki maarufu nchini Marekani na duniani, Jay- Z amezungumza namna ambavyo mtoto wake amekuwa akimpa moyo alipomwambia kuwa amekuwa akijihusisha na mapenzi ya jinsia moja
Gloria Carter aliiambia hadhira katika tuzo za GLAAD kuwa ni mara ya kwanza kuzungumza na mtu kuhusu ukweli wake
Mama wa watoto wanne alitunukiwa tuzo akitambuliwa kwa mchango wake kwenye wimbo uitwao Smile uliotolewa mwaka jana.
Alisema: ''Smile imekuwa halisia kwa sababu nilimshirikisha mtoto wangu nikimweleza mimi ni nani.''
''Mtoto wangu alilia na akasema: 'lazima maisha yalikuwa mabaya sana kuishi namna hiyo kwa muda mrefu.''
''Maisha yangu hayakuwa mabaya,''aliongeza.
''Nilichagua kuilinda familia yangu.Nilikuwa na furaha japo sikuwa huru
Zari Anunuliwa Range Rover Sport ya Mwaka 2017 na Mkenya Aliyetangaza Kumuoa Kipindi cha Nyuma
Ringtone Apoko ni msanii wa muziki wa Injili kutoka nchini Kenya ambaye kipindi cha nyuma alitangaza ni yake ya kumuoa Zari The Boss Lady, sasa muimbaji huyo amerejea tena kwenye headlines zake.
Muimbaji huyo ametangaza kuwa amemnunulia Zari gari aina ya Range Rover Sport ya mwaka 2017, hii ni baada ya kupata taarifa kuwa Zari siku si nyingi atakuwa nchini Kenya.
Soma Pia; Baada ya kuachana na Diamond, msanii wa Kenya ajitosa kwa Zari
Pia ameeleza kufurahishwa mara baada ya kumuona Zari akiwa kanisani na kumtaka kuendelea hivyo hivyo. Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;.
Dear Zari, I know you are coming to Kenya anytime from now. I take this opportunity to welcome you to my beloved country.
I checked and I realised that you were in church ⛪ on Sunday am happy because it’s only in Jesus that you won’t be hurt like Diamond did. Pleaaaase stay in church and in God. You recently posted on your IG that you wanted a Range Rover OK I took note and I want to let the world know today that I have bought you a brand new Range Rover sport 2017 model.
Am sorry I know you wanted white but I only managed a black one in color. Please arrange how to pick your key🔑 b4 you leave. While you in Kenya if you need anything let me know I will make sure it’s done for you.
Wiki iliyopitia Zari aliweka wazi kununua gari aina ya Range Rover Spor na kuibuka stori kuwa huenda mrembo huyo kapata mwanaume ambaye ameamua kumuhudumia vilivyo hata hivyo alikanusha hilo.
Zari kwa sasa anasema yupo single mara baada ya kuachana na mzazi mwenzie, Diamond Platnumz ambaye walijaliwa kupata watoto wawili, Tiffa na Nilan.
Msanii maarufu kutokea +254 Kenya Prezzo amethibitisha kumaliza beef lake na msanii mwenzake ambaye kwa sasa ni Mbunge katika jimbo la Starehe Charles Njagua maarufu kama “Jaguar “ na kulithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram.
“Kama wengi mnavojua mimi na ndugu yangu @jaguarkenya tulkuwa na friction miaka nenda, miaka rudi ila Mungu alitupatanisha tukaamua kusahau yalio pita na focus kwa ya lio mbele. Iam glad we burried the hatchet now lets put in work my brother Bless up #Rapcellency“
Alikiba Kiboko Azindua Kinywaji Chake Siku ya Harusi Yake
Alikiba Kiboko Azindua Kinywaji Chake Siku ya Harusi Yake
Msanii wa Bongo Fleva, Alikiba ametumia sherehe ya harusi yake kuzindua rasmi kinywaji chake kinachofahamika kwa jina la Mofaya katika ukumbi wa Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ambako harusi hiyo ilikuwa ikifanyika usiku wa kuamkia leo Jumatatu.
Harusi ya Alikiba Kiboko Viongozi wa Serikali Wamiminika Ukumbini
Harusi ya Alikiba Kiboko Viongozi wa Serikali Wamiminika Ukumbini Mama Salma Kikwete Ummy Mwalimu Waudhuria Kigwangala Atoa Zawadi Hii
Usiku wa jana imefanyika sherehe nyingine ya harusi ya Alikiba na mkewe Aminah Rikesh Ahmed na mdogo wake Abdu Kiba na Ruwayda katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Sherehe hiyo ilifaana zaidi baada ya kuhudhuriwa na watu lukuki wakiwemo wazazi wa wana ndoa wote na watu maarufu pamoja na viongozi wa serikali akiwemo mke wa rais wa awamu ya nne, Mama Salma Kikwete, Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu, Naibu Waziri wa Kazi, Anthony Mavunde, Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangalla na Gavana wa mji wa Mombosa, Hassan Joho ambaye pia ni mtu wa karibu wa msanii Kiba.
Mama Salma KKikwete (kushoto) akiwa na Waziri wa Àfya, Ummy Mwalimu
Katika sherehe hiyo Waziri Kigwangala amewataka maharusi wote kuchagua sehemu yoyote ya kitalii ndani ya Tanzania kwenda kufanyia fungate yao na yeye atagharamia kila kitu.
Kampuni ya Uber imesaini mkataba na Msanii Idris Sultan kuwa Balozi wake nchini Tanzania mwaka 2018
Shughuli hiyo imefanyika katika mgahawa wa kifahari wa Akemi jijini Dar es Salaam. Tangu mwanzoni mwa zoezi hili, tulifanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba tunampata balozi mwenye ufuasi mkubwa na atakayeiletea Uber ufanisi nchini Tanzania,amenukuliwa Bi.Elizabeth Njeri,
Meneja wa Masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki. Idris Sultan ni mcheshi na ni msanii ambaye hafanyi mambo yake kwa mazoea, pia anaheshimika katika tasnia ya uchekeshaji,tamthlia, na utangazaji wa vipindi vya redio. Tuna imani kwamba Idris atailetea Uber tija kubwa kwa sababu ni mzalendo kweli kweli - yeye ni kielelezo cha Utanzania na anawasiliana na mashabiki wake kupitia mitandao ya jamii kila wakati. Hizi ndizo sifa tunazosistiza tunapotaka kuwa na mkataba na mabalozi wa kampuni yetu kwa sababu zinasaidia sana katika kuonesha kwamba tunajali maslahi ya wasafiri
na madereva wanaotumia mfumo wetu nchini Tanzania. Akizungumza kwenye hafla hiyo Bw Alfred
Msemo; Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, alisema; “Kampuni ya Uber inajituma kutumia uwezo wake kupitia oparesheni zake kimataifa ili kuwa karibu na wateja wake humu nchini. Mchango wa Idris Sultan katika muziki wa Tanzania unaendana na dhamira yetu ya kujenga kampuni ya kimataifa inayogusa maisha ya madereva na wasafiri wanaotumia mfumo wetu hapa nchini. Tutaendelea kuwahudumia wasafiri wetu sambamba na kutoa fursa za ajira kwa madereva wanaotumia mfumo wetu. Idris alifurahi sana alipotangazwa kuwa Balozi wa Uber nchini Tanzania;
“Nimefurahi sana na ni heshima kubwa kwangu kupata fursa hii adimu ya kushirikiana na Uber,kwa sababu mimi nishabiki mkubwa wa mapinduzi yaliyoletwa katika sekta ya usafiri kupitia kwa mfumo wake kote duniani. Nimefurahi kuona jinsi Uber imepata umaarufu jijini Dar es Salaam, binafsi mara nyingi mimi hutumia usafiri wa uberX nikiwa na marafiki zangu kwenye mitoko yetu ya jioni na sasa wamaleta huduma nyingine ya bajaji; uberPOA ambayo nina hamu sana kuitumia - utaniona hivi karibuni. Uber inaendelea kubadilisha maisha ya maelfu ya madereva jijini Dar es Salaam sambamba
na kuwapa wasafiri uhuru wa kuchagua usafiri wanaotaka. Nimefurahi sana kuwa sehemu ya kampuni ambayo inajituma kuleta mabadiliko chanya katika maisha yetu. Baadaye kwenye hafla hiyo, Idris alipanda jukwaani na kuwatumbuiza mashabiki, wanahabari,na wafanyakazi wa Uber kwa kionjo cha kazi yake ya uchekeshaji. Msanii huyo na mshindi wa zamani wa shindano la Big Brother
Africa alivunja mbavu za umati huo kwa vichekesho vyake. Tangazo hili linakuja siku chache tangu Uber ilipo tangaza kushirikiana na Tigo kwenye mpango ambao wateja wa Tigo wanapata bando za bure wanapotumia programu ya Uber. Ushirikiano huu wa kipekee nchini Tanzania umekuwa na manufaa makubwa kwa wasafiri na madereva wanaotumia Uber na umechochea wasafiri na madereva zaidi kujiandikisha kutumia programu ya Uber nchini Tanzania.
There is a famous quote about the rich being different from “you and me.” But, it turns out that, in the afterlife, the rich and famous aren't much different from us common folk. Like the rest of us, if a star has died an untimely death or was surrounded by controversy, it's possible that they won't be able to let go of this mortal life. Here are seven of the most well-known celebrity “ghost stories” out there:
1. Michael Jackson
When Michael Jackson died he left a complicated legacy. Sure, he has many fans, but legal scandals haunted his career and criminal accusations plagued his legacy. For many it was complicated to think of their childhood icon and all the very many accusations against him. In other words, he was a man with unfinished business. So it’s not shocking that many claimed to have seen his ghost at his home (The Neverland Ranch) back in a Larry King segment in 2009.
2. Lucille Ball
The comedian and all around legend in Hollywood is often seen hanging around the site of her former Beverly Hills home (it was destroyed and a replacement was built on the lot), especially in the attic where noises and thumps are the norm. Even a funny ghost is pretty scary when you think about it!
3. Jean Harlow
She was the first real bombshell, but her life was terribly tragic. She died at only 26 of kidney disease and was, for a time, the wife of a man who allegedly abused her. Her husband, an MGM executive, later shot himself in their bedroom. One family who lived there in the 1970s said they smelled perfume, heard a woman crying and finally, heard a woman whisper: "Please help me."
4. Heath Ledger
He died tragically at age 28 of an accidental drug overdose. Since then, many have claimed to contact his ghost through mediums and his ex, Michelle Williams, even said she saw him as a ghost since his death. Dying so young undoubtedly leaves unfinished business. And tragedies often beget hauntings.
5. John Lennon
Many have claimed encounters with the spirit of John Lennon. At the Dakota where he lived in NYC, among other places. Maybe it’s that he was so beloved, people want him back. Or maybe it’s something more. Certainly his death was violent and sudden enough to warrant a potential lingering essence.
6. Marilyn Monroe
Over the years, many have claimed to see the ghost of the beautiful actress with the tragic back story. She has been spotted in hotels, at séances, and in the home in Brentwood, California where she died.
7. Orson Welles
The spirit of the Hollywood legend has been said to enjoy brandy at the Sweet Lady Jane bakery on Melrose Avenue in Los Angeles.
Shamsa Ford: Diamond Endelea Kuwatumia Hao Wanawake Maana Hawajielewi, Lakini Kumbuka Kutumia Kinga
Muigizaji wa Bongo movie na mfanyabiashara Shamsa Ford Amefunguka na kudai kuwa sio kweli kwamba Diamond anawadhalilisha wanawake ambao wanatoka nao kimapenzi kwa kusambaza video zao mtandaoni.
Diamond alizua gumzo hili siku ya jana bada ya video zake kusambaa mtandaoni akiwa na Hamisa Mobetto chumbani wakikumbatiana na wakati huo huo akiwa na binti wa kizungu wakiwa pamoja chumbani pia Wakila denda na uchafu mwingine.
Kwenye mahojiano aliyofanya na Bongo 5 Shamsa aliulizwa nini maoni yake juu ya jambo hilo na alifunguka na kumtaka Diamond aendelee kutoka na wanawake tofauti tofauti kwa kuwa hawajitambui huku amtahadharisha kutumia kondom ili kuepuka magonjwa na zinaa.
"Mwanaume hawezi kukufanya mwanamke ukawa chombo cha starehe ...inategemea mwenyewe na akili yako,kama unataka kuchezewa utachezewa kama unataka kuwa mwanamke wa muhimu kwake utakuwa inategemea mwenyewe unajiweka wapi
"Kwa hiyo mimi siwezi kumlaumu Diamond kama anawatumia maana wenyewe ndio wameweka mazingira hayo kwa nini asitumie nafasi? Ila mimi namshauri Diamond awale tu hao wasichana ila akumbuke kutumia kinga maana magonjwa mengi”.
Diamond Platnumz Amefikishwa Polisi Kisa Video Zisizo na Maadili
BUNGENI: Msanii Naseeb Abdul Maarufu kama Diamond Platnumz amefikishwa Polisi jana kuhojiwa kutokana na kusambaza kwa video zake zisizo na maadili katika mitandao ya kijamii
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa Bungeni wakati akijibu swali juu ya kanuni za maudhi ya Mitandaoni
Aidha, Dkt. Mwakyembe amesema Msanii Faustina Charles (Nandy) naye atahojiwa na Polisi kufuatia video yake ya faragha akiwa na Msanii mwenzake Billnas kusambaa mitandaoni.
Wasanii wa Kitanzania wapeperusha Vizuri Bendera Wanyakua Tuzo Ghana
Muigizaji wa filamu nchini Tanzania, Yvonne Cherry maarufu kwa jina la Monalisa ameshinda tuzo ya The African Prestigious Awards (APA) 2017 kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Kike barani Afrika.
Tuzo hizo zilizotolewa usiku wa kuamkia jana mjini Accra nchini Ghana ambapo waigizaji wengine kama Ray na Mzee Majuto nao walikuwa nominated kwenye tuzo hizo, ambapo Ray Kigosi pia ameshinda tuzo ya muigizaji bora wa kiume barani Afrika.
Kwa upande mwingine, Mtanzania Moise Hussein ameshinda tuzo hizo kwenye kipengele cha mpiga picha bora barani Afrika kwa mwaka 2017.
Bilnass Amjibu Nandy...Adai Nandy Alianza Toka Jana Kuvujisha Picha na Leo Video...Afunguka Makubwa
From Bilnass:
"Jana ilikuwa Siku Yangu Nzuri Ya Kumbukumbu na Siku Ya Kuzaliwa Kwangu,
Siku Moja Nyuma alinitafuta Nandy ambae tuliwahi kuwa kwenye Mahusiano Ya Pamoja kwa kipindi, akaniomba nimtumie picha zangu na yeye za Pamoja a post kwajili ya Birthday Yangu nikamueleza ukweli Sina Memory yeyote ya pamoja na Wewe Sababu tulivyoachana nilifuta na Naheshim Mahusiano niliyonayo Sasa ! Kwa Bahati Mbaya nilichelewa Kuamka Jana nikakuta sim Nyingi za Interviews I thought ni kwajili ya Birthday Wishes....
Then nikakutana na interview zinazotaka nieleze juu ya picha iliopostiwa na Nandy,Sikuwa na jibu Sababu sie niliepost na sikuwa nayo hata kwenye backup hizo picha nikafuatilia nikakuta picha imepostiwa na @reyjons na @officialnandy mwenyewe! Nikamtafuta Reyjons kwa WhatsApp kwanini umepost vile ?madhara yake si unayajuwa....akaniambia ametumwa na Nandy Mwenyewe,then ikapostiwa na Nai Official Ambae ni rafiki wa Nandy !ikaniletea Shida sana kwa Mpenzi wangu nilijitahidi kujielezea lakini Swali lilikuja hata kama mmeachana anapata hiyo authority ya kupost ??ikabidi nimtafute Nandy na kuhoji kwanini upost picha kama Ile?? Akasema ni Gift yako ya Birthday nimetaka utrend! Sikuelewa nikamuuliza umetazama upande wangu lakini ??akatuma Voice Notes ambayo ninayo akielezea kwanini kapost ile picha na Mipango ya utoaji wake wa Wimbo Mpya !
Uzuri Nina hyo Voice notes na Baadhi ya sms sababu Mawasiliano tulikuwa tunafanya Snapchat !kwa kinywa Chake Mwenyewe alinieleza wamepanga kick kubwa na team yake itanihusisha mimi nikahoji Sana ni kick gani hyo ?nimpige ASLAY kwenye video yake kwa Utani !
Hakujibu tena text leo nimeamka kama Saa 8 au Saa 9 Mchana maaana nililala Saa 2 asubuhi ! Nilivyoamka Nimekuta sim Nyingi Za Ndugu,Jamaa,Watangazaji na Marafiki lakini nilikuwa nashindwa kupokea Sababu ya tatizo la WhatsApp Call Hapa UAE, nikabahatika Kuiona hyo VIDEO kiukweli Nimelia Sana, Hakuna kitu kinaniuma Kama Mama Yangu Mzazi anavyonipenda akutane na tukio kama hili...Nikajaribu Kumtafuta Manager wangu Mchafu afanye Mawasiliano na Nandy kuona imekaaaje lakini Nandy alisema hajui lolote na aliwahi kunitumia hii VIDEO kitu Ambacho sio Kweli hata kidogo ,Niko na Akili zangu Timamu
Niko na Akili zangu Timamu Nasema kama kuna njia yeyote aliwahi kunitumia video hyo ama kwa WhatsApp au popote niko teyari kuwajibika, Sijawahi kuwa na VIDEO kama hyo wala katika kipindi changu chote cha Mahusiano na Nandy hata na Ex Wangu Wengine sijawahi kudeal na Camera Faragha....Nimekwazika Sana,Naomba Radhi Wazazi na Familia Yangu, Ndugu zangu na Mpenzi wangu,Pia Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Baraza la Sananaa la Taifa,Mamlaka zote Husika, Media na Wadau Wote wa Sanaaa,Management yangu,Mashabiki zangu na Hata watoto na Familia Yangu itakayokuja kukutana na Fedhea hii !nikotayari uchunguzi ufanyike kubaini chanzo cha VIDEO Hii.....Naona sim ni Nyingi lakini siko kwenye hali nzuri hata kidogo naaamini hayo nilioyaaandika atatisha kwa sasa.... "
Ni miezi miwili imepita tokea marehemu Radio afariki February 1, 2018, Radio ambae alikuwa pamoja na Weasel wakiunda kundi la Goodlyfe kutokea nchini Uganda, msiba wa Radio uligusa watu wengi duniani.
Baada ya Radio kufariki mtuhumiwa Wamala Godfrey alias Troy anayedaiwa kusababisha kifo cha Radio alikimbia na hakuonekana kwa wiki kadhaa lakini baada ya polisi kuendesha msako wa walifanikiwa kumkamata.
Wamala Godfrey alias Troy amekiri kuwa alisababisha kifo cha Radio na kusema kuwa Radio alimponyoka mikononi mwake na kujipigiza kichwa chake chini wakiwa wanapigana haikuwa lengo lake kumuua na hivyo kuomba msamaha.
Roma Mkatoliki Akabidhiwa Cheti cha Usajili BASATA
Roma Mkatoliki Akabidhiwa Cheti cha Usajili BASATA Awapa Ujumbe Huu Wasanii Wenzake
Rapa Roma Mkatoliki leo Alhamisi Aprili 05, 2018 amekabidhiwa cheti cha usajili kutoka BASATA hii ni baada ya kupewa masharti ya kufanya hivyo na Wizara ya Habari ili aweze kufutiwa adhabu yake ya kutojihusisha na muziki kwa miezi sita.
Roma akiongea na waandishi wa habari baada ya kukabidhiwa cheti hicho, amewashukuru watu wote walipaza sauti hadi kufutiwa adhabu hiyo, pia amewaasa wasanii wenzake kuchukua hatua mapema za kujisajili.
Muigizaji Maarufu wa Filamu za Kihindi Salman Khan ...
Muigizaji Maarufu wa Filamu za Kihindi Salman Khan Amehukumiwa Miaka Mitano Jela
Muigizaji marufu wa filamu wa India Salman Khan amehukumiwa miaka mitano jela, kwa kosa la ujangili alilolifanya mwaka 1998.
Hukumu hiyo imetolewa leo na mahakama ya India baada ya kumkuta na hatia, huku waigizaji wenzake Saif Ali Khan, Tabu, Sonali Bendre na Neelam Kothari wakiachiwa huru kutokana na kutokutwa na hatia.
Salman Khan alishtakiwa kwa kosa la ujangili la kuua wanyama wawili wanaojulikana kama 'blackbucks' ambao ni jamii ya swala wa kipekee walioko nchini India, na serikali ya nchi hiyo inawatunza kwa uangalizi mkubwa.
Salman Khan alifanya tukio hilo katika kijiji cha Kankani ambako alikuwa akiigiza filamu yake ya Hum Saath Saath Hain , akiwa na waigizaji wenzake.